Thursday, 7 May 2020

CCM UBUNGO YAMPONGEZA DC MAKORI KWA UTENDAJI

...

 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori, (kushoto) akiwasilisha taarifa yake mbele ya Kamati ya Siasa Wilaya ya Ubungo, katikati ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya  ya Ubungo, Lucas Mgonja pamoja na Katibu wa wilaya hiyo, Chifu Silvester Yaredi

Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Ubungo, wakijadili taarifa ya utendaji ya Mkuu wa Wilaya

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM
 
KAMATI ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ubungo, chini ya mwenyekiti wake Lucas Mgonja, imempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori kwa utendaji wake ikiwamo vita dhidi ya ugonjwa wa corona wilayani humo.

Taarifa ilitolewa leo na Katibu wa Siasa ya Uenezi, Wilaya ya Ubungo, Mbaruku Masudi, imeeleza kuwa katika kikao hicho pamoja na mambo kilipokea taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori  ikiwamo hali ya ugonjwa wa corona, ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo kwa shule za msingi na sekondari wilayani Ubungo.


“Jana tarehe 6/05/2020  Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ubungo ilikuwa na kikao chake cha kwanza cha kawaida kwa mwaka 2020.

“Katika Kikao hicho pamoja na mambo mengine kilipokea taarifa kutoka kwa Kamisaa wa chama Mkuu wa Wilaya Kisare Makori ikiwamo taarifa ya hali ya ugonjwa wa corona katika wilaya yetu (Ubungo) na jitihada zinazofanyika.

“Ujenzi wa vyumba vya madarasa, ofisi za walimu, matundu ya vyoo na ununuzi wa viti, meza na madawati. Pia kikao kilijadili hali ya uharibifu wa miundombinu ya barabara nahatua zilizochukuliwa hasa katika kipindi hicho cha mvua,” amesema Mbaruku

Katibu huyo Mwenezi wa Wilaya ya Ubungo, amesema kuwa pamoja na hali hiyo pia walipokea taarifa ya kutoka kwa DC Makori kuhusu kupatikana kwa eneo la ujenzi wa mahakama ya wilaya, polisi, Zimamoto na Uokoaji pamoja na ujenzi wa ofisi ya Katibu Tarafa Kibamba eneo lenye ukubwa wa takribani ekari 11.9.

“Pia Kamati ya Siasa ya Wilaya chini ya Mwenyekiti Mgonja ilipokea taarifa kuhusu suala la bei elekezi ya sukari na hatua zilizochukuliwa,” amesema

Kutokana na hali hiyo amesema kuwa CCM Wilaya ya Ubungo, kimeipongeza Serikali ngazi ya wilaya na kuishauri kuongeza jitihada katika kutoa elimu kuhusu kingi dhidi ya ugonjwa wa corona ikiwamo kujilinda na janga hilo.

Pamoja na hali hiyo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo, Lucas Mgonja, alitoa wito kwa wana CCM kuendelea kushirikiana na Serikali katika kipindi hiki ili kuhakikisha maelekezo yote muhimu yanatolewa yanazingatiwa.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger