Friday, 25 December 2020

ASKARI POLISI ALIYEFUMANIA NA KUMJERUHI JAMAA GESTI AKAMATWA

...

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, ACP Pili Mande.
***
Jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma, linamshikilia Askari Polisi Keneth Mkwela, kwa kosa la kumjeruhi mwanaume mwenzake anayejulikana kwa jina la Andrew Milanzi, na kitu chenye ncha kali, baada ya kumfumania akiwa na mwenza wake kwenye nyumba ya kulala wageni.

Akizungumzia tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, ACP Pili Mande, amesema kuwa chanzo kikubwa cha Askari huyo kujeruhi ni wivu wa kimapenzi na tukio hilo lilitokea katika Kijiji cha Magagula, wilaya ya Songea mkoani humo.

"Tukio limetokea Desemba 8 mwaka huu, alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya chini ya mbavu za kushoto baada ya kutokea ugomvi na mhanga anaendelea na matibabu, kiini cha ugomvi huu ni wivu wa mapenzi baada ya mtuhumiwa kumkuta mwenza wake akiwa anaongea na mpenzi wake, na hatua za kinidhamu za kijeshi zinaendelea", amesema ACP Mande.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger