Friday, 21 December 2018

VIONGOZI WAMVAA MKUU WA MKOA ANAYEDAIWA KULAZWA MAKABURINI NA WACHAWI WA IRINGA

...

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi

Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi kumtaka Katibu wa BAVICHA Kinondoni, Hilda Newton kujisalimishakatika kituo cha polisi Iringa siku ya leo, kwa kusambaza taarifa zenye ujumbe wa kwamba huko Iringa 'Ali Happi amelazwa makaburini, viongozi wamekimkingia kifua kuwa hatajisalimsha.

Hapi amekutana na vikwazo kutoka kwa viongozi mbalimbali baada ya sakata hilo kusambaa kwenye mitandao likimuhusisha, Hilda kuchapisha habari iliyosema,"Watu Iringa nimewanyoshea mikono . Naambiwa mwezi 1 uliopita, Ally Happi alikuwa amelala nyumbani kwake ilipofika alfajiri alijikuta amelala makaburini akiwa amevaa boksa pekee ikabidi akimbilie Dar alafu tangu siku hiyo mpaka leo hajarudi Iringa na kaomba abadlishiwe kituo cha kazi".

Baada ya habari hiyo kusambaa katika mitandao Disemba 17, Hapi alimtaka kiongozi huyo wa Baraza la Vijana Chadema kuripoti kituo cha polisi Iringa Desemba 21.

"Mlio karibu na huyu binti mfupi wa BAVICHA mkumbusheni kesho tarehe 21 saa 2 asb ndio mwisho wa kujisalimisha kwa hiyari kwa RPC Bwire Central Police Iringa" Ally Hapi.

Baada ya kauli hiyo ya Hapi katika ukurasa wake wa Twitter, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche ameandiaka, "Mtume Bwire amtafute hatajisalimisha 'unless' useme sheria gani inakupa mamlaka wewe 'kumsummon'!!!. Tumia madaraka vizuri, bado wewe ni kijana, lakini kwasababu yamekulevya hautaelewa".


Naye Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amemjibu Kiongozi huyo kwamba, "Kwanini unakosa busara?. Unamwita mtu mfupi? Halafu wewe ni Kiongozi?, huna mamlaka ya kumwita Mtu yeyote kuripoti Polisi. Hatakuja na hutafanya kitu. Jifunze hekima za uongozi Ally. Usiwe na kibri kwani kibri si maungwana. Sasa Hilda hatatii amri yako batili. Tuone utafanya nini".

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA, Patrick Ole Sosopi amemjibu Hapi kwamba, "Nafikiri this time utaelewa Job Description (majukumu ya kazi) yako vizuri kwa sababu tunafahamu hujui, semina elekezi za majukumu yenu mlio wengi hajapewa. Wewe utakuwa Mwalimu wa wenzako kupitia hili, Jeuri ya Madaraka uliyonayo na kutumia vyombo vya dola vibaya, Hilda Newton hatokuja tuone".

Kwa upande wa Mbunge wa Iringa, Peter Msigwa amesema, "Hayo ni matumizi mabaya ya madaraka! Uongozi wa kutisha tisha watu umepitwa na wakati, kama umekosewa fuata tatatibu za kisheria , huna madaraka ya kukamata kamata watu ovyo!".

Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA), Zubeda Sakuru naye amemjulisha kiongozi huyo kwamba, "Hatokuja na hutofanya kitu. Mweupe wewe".

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger