Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi ameliagiza Jeshi la polisi mkoani humo kufanya uchunguzi juu ya tuhuma zilizosambaa mtandaoni zikimuusisha na imani za kishirikina.
Hapi amesema hadi leo Ijumaa Desemba 21, 2018 jeshi la polisi limegundua aliyetunga uzushi huo ni Katibu wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) wilaya ya Temeke, Hilda Newton.
“Nimeagiza popote alipo huyo katibu wa Bavicha akamatwe atoe maelezo ya alichokizusha mtandaoni na athibitishe alichokiandika," amesema Hapi.
Hapi amesema amepitia akaunti ya Hilda Newton na kugundua ni tabia yake kuzusha vitu vya uongo mtandaoni.
Amesema kumtaja kwa kimo chake hajaona kama ni udhalilishaji bali alitofautisha watu waliokuwa katika picha hiyo.
"Nimemtaja kuwa ni mfupi na kweli ni mfupi ukilinganisha na mtu aliyekuwa amesimama naye katika picha niliyoiposti kumtaka akajisalimishe."
Awali baada ya kutakiwa kujisalimisha, Hilda alinukuliwa akisema kwamba hatokwenda polisi kujisalimisha kama alivyotakiwa na Hapi.
Na Berdina Majinge, Mwananchi
0 comments:
Post a Comment