Arusha. Mkutano wa wakuu wa nchi Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ambao ulikuwa umepangwa kufanyika jijini Arusha hapa nchini umefutwa kwa mara ya pili ndani ya wiki tatu. Mkutano huo wa marais wa nchi wanachama wa EAC ambazo ni Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi Sudan Kusini ulitazamiwa kufanyika Desemba 27. Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Christophe Bazivamo, amesema, “Ni rasmi sasa, mkutano huo hautafanyika Desemba 27 kama ilivyokuwa imepangwa. Tarehe na mahala pa kufanyika mkutano huo wa 20 wa wakuu wa EAC itatangazwa baadaye.” Kikao cha mawaziri…
0 comments:
Post a Comment