Na Bakari Chijumba (Beca Love),Mtwara. Baada ya kufungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),wasanii Diamond Platnumz na Rayvanny wamejitokeza hadharani na kuomba radhi kwa kuimba wimbo wa “Mwanza” uliofungiwa, huku wakiwasihi wasanii wenzao kuwa mabalozi wazuri wa utamaduni wa Tanzania. Kupitia kipande cha video chenye sekunde 54 ambacho kimewekwa kwenye ukurasa wa Instagram wa Diamond pamoja na ule wa RayVany leo 21 Dec 2018, wasanii hao wameonekana wakiongea kwa masikitiko na hisia kali na kujutia walichokifanya. “Kwa unyenyekevu mkubwa tunaomba radhi Serikali, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,…
0 comments:
Post a Comment