Bujumbura, BURUNDI. Shirika lisilo kuwa la kiserikali la Avocates sans frontières limesitisha shughuli zake nchini Burundi kufuatia sheria mpya ya nchi hiyo kuhusu mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali. Hili ni shirika la kwanza la kigeni nchini Burundi kuchukuwa uamuzi huo, siku chache kabla ya muda wa mwisho uliowekwa na serikali kuanza kutumika kwa vigezo vya wafanyakazi kuwa kuwepi uwiano wa 60% ya Wahutu na 40% ya Watutsi. Mamlaka nchini Burundi ilichukuwa uamuzi wa kusitisha shughuli za mashirika yote ya kigeni na kupewa muda hadi Desemba 31 ili kuzingatia sheria hiyo…
0 comments:
Post a Comment