Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya
Juu imekamilisha zoezi la kurekebisha fomu za maombi ya mikopo kwa
waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017. Zoezi hilo lilianza tarehe 3 na kumalizika tarehe 7 Oktoba 2016.
Kwa sasa Bodi inaendelea na hatua za
awali za upangaji wa mikopo ambapo taarifa za wanafunzi watakaopangiwa
mikopo zitatolewa kwenye tovuti ya Bodi www.heslb.go.tz siku chache zijazo.
NB: Bodi inawakumbusha waombaji mikopo wote kuwa makini na watu wasio waaminifu wanaoweza kutumia fursa hii kujipatia fedha isivyo halali.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
0 comments:
Post a Comment