Tume
ya vyuo Vikuu (TCU) inautangazia Umma kuwa baada ya kukamilisha mchakato wa
maombi ya waombaji wa vyuo vikuu, vyuo Vikuu Vishiriki na Taasisi za elimu ya
juu kwa awamu ya kwanza, ya Pili na ya tatu, na matokeo ya waombaji wote
waliofanikiwa kupata nafasi vyuoni kukamilika, Tume ya vyuo Vikuu imebaini kuwa
bado kuna waombaji takribani 5,301 ambao bado wako kwenye mfumo na
hawajakamilisha maombi yao.
Tume imebaini pia kuwepo kwa idadi
kubwa ya waombaji hasa wenye Stashahada ambao hawakuomba kabisa kutokana na
matokeo yao ya mitihani kuchelewa kufika Baraza za Vyuo Ufundi (NACTE)
Awamu hii itawahusu:
•
Waombaji
ambao bado wako ndani ya mfumo ambao hawajapata nafasi
•
Waombaji wapya ambao hawakuwahi kuomba awali;
na
•
Waombaji walio na sifa linganifu ambao
hawakukamilisha taratibu za uombaji hapo awali
Kutokana
na sababu tajwa hapo juu, tume inautangazia Umma kuwa itafungua Mfumo (CAS) kwa
siku tatu tu, kuanzia Jumatatu tarehe 24 hadi Jumatano tarehe 26 Oktoba
2016 ili kuruhusu Makundi tajwa hapo juu kuingia kwenye mfumo kutuma
maombi.
Waombaji wa awamu Nne
wanasisitgizwa kuzingatia yafuatayo:
•
Kuhakikisha
wanaomba kozi walizo na sifa stahiki
•
Kuhakikisha wanakamilisha maombi yao
kiufasaha
•
kuhakikisha wanajiridhisha na nafasi zilizopo
kwa kuzingatia viwango vyao vya ufaulu.
Aidha Tume inapenda kuujujulisha Umma kwamba kozi zote
zosizo onekana kwenye mfumo kwa sasa kuwa zimejaa.
Baada ya tarehe tajwa hapo juu tume itafunga rasmi zoezi
la udahili kwa mwaka 2016/17 ili kuruhusu mchakato mingine ya Bodi ya Mikopo na
Vyuo kuendelea.
Kaimu Katibu Mtendaji
Tume
ya Vyuo Vikuu Tanzania 21/10/2016
0 comments:
Post a Comment