Tuesday, 18 October 2016

Basi la Barcelona Lapata Ajali na Kuua Watu 10 Mkoani Lindi

...

Watu 10 wamefariki dunia na wengine 44 wamejeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Barcelona walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Dar es Salaam kwenda mkoani Lindi  kupata ajali eneo na Miteja mkoani Lindi.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renata Mzinga imesema kuwa chanzo cha ajali hiyo kimetokana na tairi ya gari ya upande wa kushoto kupasuka na kutokana na mwendo wa kasi wa basi hilo, dereva alipoteza uelekeo ndipo likapinduka.

Pia Kamanda Mzinga amesema kuwa wamechunguza na kugundua kua licha ya kuwa basi hilo lilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 48, wakati basi hilo linapata ajali kulikuwa na abiria 54 kitu ambacho ni kosa kisheria.

Aidha, Kamanda Mzinga amesema kuwa bado wanaendelea na uchunguzi kuweza kubaini alipo dereva ili kuweza kufahamu ni kipi hasa kilichotokea. Hadi sasa wanamshikilia kondakta wa basi hilo lakini bado hajaweza kuelezea tukio halisi.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger