Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Thomas Mashali, hatunaye.
Taarifa
zinaeleza ameuwawa kwa kupigwa risasi na mwili wake kuokotwa vichakani
maeneo ya Kimara jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.
Yassin
Abdallah maarufu kama Ustaadhi, mmoja wa viongozi wakongwe wa mchezo wa
ngumi amethibitisha na kusema mwili wa Mashali upo kwenye chumba cha
kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili jijini Dar es
Salaam.
"Tumethibitishiwa hizo taarifa za majonzi kabisa, mwili upo Muhimbili na msiba upo kwao Tandale," alisema Ustaadhi.
"Tumethibitishiwa hizo taarifa za majonzi kabisa, mwili upo Muhimbili na msiba upo kwao Tandale," alisema Ustaadhi.
0 comments:
Post a Comment