Mkazi wa Mahembo Manyanda Manyilizu (40) ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mdogo wake baada ya kumfumania akiwa na mkewe.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Dismas Kisusi
alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi katika Kijiji cha Mawemilu.
“Manyilizu
alimkuta mdogo wake akifanya mapenzi na mkewe, alivyomuhoji, mdogo wake
alichukua kitu akampiga nacho kichwani hivyo alifariki dunia wakati
akiendelea na matibabu katika zahanati ya Kijiji cha Mawemilu,” alisema
Kisusi.
Alidai mtuhumiwa na mwanamke walikimbia baada ya kufanya tukio hilo.
Katika tukio jingine, watu wawili wameuawa kwa kupigwa mawe na marungu kisha miili yao kuchomwa moto na wananchi.
Kisusi alisema tukio hilo lilitokea juzi katika Kijiji cha Shimba wilayani Kahama.
Kisusi
alisema watu hao walituhumiwa kuwa ni majambazi baada ya kumvamia
Mchongaraji Ndalawa (65), akiwa amelala nyumbani kwake wakimtaka awape
fedha.
“Alivyosema hana walimkata kwa panga kichwani, ndipo wananchi walijichukulia sheria mkononi kwa kuwaua,” alisema.
Majeruhi huyo amelazwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama na hali yake inaendelea vizuri.
0 comments:
Post a Comment