Wabunge wa upinzani, Tundu Lissu na Esther Bulaya wamesimamishwa kutoshiriki shughuli za bunge kwa mikutano miwili ya bunge hilo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na kung’ang’ania kurushwa matangazo ya moja kwa moja ya bunge hilo.
Adhabu hiyo iliyotolewa jana jioni bungeni mjini Dodoma inamaanisha kuwa wabunge hao hawataingia bungeni hadi mwaka 2017.
“Mimi na Halima tunasimamishwa shughuli za bunge mpaka mwezi Septemba,” alitweet Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini.
“Wabunge wote wa upinzani wamepewa onyo kali kwa kung’ang’ania kutoka bunge lioneshwe moja kwa moja na shirika la TBC.”
Wabunge wengine waliopewa adhabu na kamati ya maadili, haki na madaraka ya bunge ni Pauline Gekuli na Godbless Lema ambao hawatahudhuria vikao vyote vya mkutano wa tatu.
Mbunge John Heche amepewa adhabu ya kutoshiriki vikao 10 vya mkutano wa tatu.