WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania ina mpango wa kujenga njia ya
umeme kutoka Mbeya hadi Zambia kupitia Tunduma ili kupunguza tatizo la
umeme linaloikabili nchi hiyo.
“Serikali
ya Tanzania inajenga njia ya umeme ya msongo wa KV 400 kutoka Iringa –
Dodoma – Singida – Shinyanga ambayo ni sehemu ya mradi mkubwa wa umeme
unaolenga kuunganisha Zambia, Tanzania na Kenya,” amesema.
Amesema
upembuzi yakinifu kwa ajili KV400 kutoka Iringa hadi Mbeya
umekwishakamilika tangu mwaka 2012, na hivi sasa Serikali inatafuta
fedha kwa ajili kuunganisha kipande cha kutoka Mbeya na gridi ya Taifa
ya Zambia.
Waziri
Mkuu ambaye anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk.
John Pombe Magufuli, ametoa ufafanuzi huo jana mchana (Jumanne, Mei 24,
2016) wakati akichangia hoja kwenye mjadala wa wakuu wa nchi na Serikali
uliohusu Nishati na Mabadiliko ya TabiaNchi kwenye ukumbi wa mikutano
cha kimataifa wa Mulungushi.
Alisema
ili kukabiliana na changamoto ya nishati barani Afrika, nchi za bara
hili zinahitaji kuwa na fedha ama mitaji, teknolojia ya kisasa na
wataalamu wenye ujuzi wa kutosha jambo ambalo amesema ni gumu
kulikamilisha kila nchi peke yake.
Alisema
ili kukaribisha wawekezaji kwenye sekta ya umeme, Tanzania inafanyia
marekebisho sheria zake ili kuruhusu uwekezaji kwenye sekta hiyo.
Akizungumzia
kuhusu hali ya nishati Tanzania, Waziri Mkuu alisema Tanzania
imebarikiwa kuwa na gesi asilia yenye ujazo wa futi trilioni 57.25
(tcf), makaa ya mawe yenye uhjazo wa tani bilioni 1.9 (asilimia 25
imevumbuliwa), umeme wa nguvu ya maji wa gigawati 4.7 ambazo ni asilimia
12 tu ndiyo inatumika. Pia alisema Tanzania ina deposits za urani yenye
ujazo wa ratili milioni 200 (200 million pounds), joto la ardhini
(geothermal) linaloweza kuzalisha umeme wa megawati zaidi ya 5,000.
“Hivyo ni mbali na vyanzo vya umeme utokanao ua upepo na jua,” alisema.
Akizungumzia
kuhusu usambazaji wa umeme vijijini, Waziri Mkuu alisema Tanzania
kupitia REA imefanikiwa kusambaza umeme kwenye asilimia 52 ya vijiji
vyote na inatarajia kufikia asilimia 90 ifikapo mwaka 2025.
Akishiriki
mjadala huo, Makamu wa Rais wa Nigeria, Bw. Yemi Osinbajo alisema bara
la Afrika linahitaji kuwa na vyanzo vikubwa vya umeme kama kweli
linataka kufanikiwa kukamilisha kuwa na viwanda vya kutosha.
“Hatuwezi
kuwaza kuwa na viwanda vingi wakati tukitegemea umeme wa nguvu ya jua
peke yake… huu unahitaji uwekezaji mkubwa na eneo kubwa la kuweka
mitambo,” alisema.
Naye Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw. Carlos Agostinho do Rosário
Akishiriki
mjadala huo, Makamu wa Rais wa Nigeria, Bw. Yemi Osinbajo alisema bara
la Afrika linahitaji kuwa na vyanzo vikubwa vya umeme kama kweli
linataka kufanikiwa kukamilisha kuwa na viwanda vya kutosha.
“Hatuwezi
kuwaza kuwa na viwanda vingi wakati tukitegemea umeme wa nguvu ya jua
peke yake… huu unahitaji uwekezaji mkubwa na eneo kubwa la kuweka
mitambo,” alisema.
Naye
Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw. Carlos Agostinho do Rosário alisema
masuala ya nishati yanahitaji uwekezaji mkubwa kwa hiyo akashauri
makampuni kuungana kwenye uwekezaji na kuibua miradi ambayo ina tija
(feasible and viable).
Waziri
Mkuu amefuatana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Asantu Kijaji,
wachumi kadhaa pamoja na wataalamu wa sekta ya fedha.
0 comments:
Post a Comment