TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amesema mkoa wa Mwanza unategemea
kupokea Tani 500 za Sukari zitakazo ingia katika mkoa huu zikitokea
kiwanda cha sukari cha Kagera Sugar tarehe 24, Mei, 2016, ambazo
zinaingizwa mkoani hapo na muagizaji na Msambazaji P.H Shah.
Hata
hivyo mkuu wa mkoa ameonya watu watakao uza sukari hiyo kinyume na bei
elekezi kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja nakufikishwa
katika vyombo vya dola.
Mongella
amesema pia kwamba, kupitia kamati yakushughulikia sukari, tayari
wametoa maelekezo kwa Wakuu wa wilaya jinsi yakushughulikia suala la
sukari na kwamba wasambazaji wote katika Wilaya lazima wazingatie
maelekezo bila kuvunja utaratibu utakao wekwa.
Mahitaji
ya sukari katika mkoa wa Mwanza ni Tani 1,500 kwa wiki kwa matumizi ya
kawaida kwa wananchi wake, hivyo kuwasili kwa tani 500 itasaidia
kupunguza uhaba wa sukari unao ukabili mkoa huu kwa sasa..
Hata
hivyo mkuu wa mkoa amewatoa wanachi hofu juu ya sukari kwakusema,
tayari viwanda vya hapa nchini vimekwisha anza uzalishaji wa sukari na
kwamba muda si mrefu tatizo la sukari litapungua kama sio kuisha kabisa.
Imetolewa na Atley J. Kuni
Afisa habari na Mahusiano, Ofisi ya mkuu wa Mkoa
MWANZA -24, Mei 2016
0 comments:
Post a Comment