Monday, 15 February 2016

Ugonjwa sugu wa figo (Chronic Kidney Disease)-2

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
fnalkidney-comp_10878482UGONJWA WA FIGO HUSABABISHA KISUKARI
Leo tunaendelea kuelezea ugonjwa sugu wa figo kwa kuanzia na jinsi unavyosababisha matatizo ya kisukari. Endelea.
Kisukari cha aina ya 1 na ya 2 husababisha hali iitwayo kisukari cha figo au kwa kimombo Diabetic Nephropathy. Shinikizo la damu kama lisipodhibitiwa vyema, baada ya muda fulani husababisha madhara katika figo.
Pia magonjwa ya kurithi ya figo kama vile Polycystic Kidney Disease (PKD). PKD huambatana na hali ya kuwa na vimbe ndogondogo zilizojaa maji katika figo.
Vimbe hizi hufanya figo ishindwe kufanya kazi zake sawasawa na hivyo kusababisha ugonjwa sugu wa figo.
Vilevile matumizi ya kila siku ya muda mrefu ya baadhi ya madawa ya kutuliza maumivu kama vile Ibuprofen au Acetaminophen yanaweza pia kusababisha ugonjwa sugu wa figo. Hali hii huitwa kitaalamu Analgesic Nephropathy.
Matumizi ya baadhi ya madawa kama Antibiotics za Aminoglycosides kama vile Gentamicin pia husababisha madhara katika figo na hatimaye ugonjwa sugu wa figo.
Kadhalika hali ya mishipa ya damu inayosambaza damu kwenye figo kuzeeka, kuwa migumu kiasi cha kushindwa kutanuka na kusinyaa. Atherosclerosis husababisha upungufu mkubwa wa damu katika figo husika, kwa kitaalamu hali ambayo inaweza pia kusababisha madhara zaidi kwa figo na hatimaye ugonjwa sugu wa figo.
Magonjwa kama vijiwe katika figo, kuvimba tezi dume, kuziba kwa njia ya mkojo pamoja na saratani, vyote vinaweza pia kusababisha madhara katika figo na hatimaye kusababisha ugonjwa sugu wa figo.
Vyanzo vingine vya ugonjwa sugu wa figo ni pamoja na maambukizi ya virusi vya Ukimwi ambayo husababisha hali inayoitwa HIV Nephropathy, ugonjwa wa upungufu wa damu mara kwa mara yaani Sickle Cell, unaweza kusababisha kuziba kwa mirija inayosambaza damu kwenye figo au upungufu wa damu kwenye figo.
Pia matumizi ya madawa ya kulevya, maambukizi sugu katika figo na saratani za figo. Mtu aliye na mojawapo ya vitu au magonjwa haya ana hatari kubwa ya kupata ugonjwa sugu wa figo.
USHAURI
Wenye matatizo haya, hawana budi kuhakikisha kuwa figo zao zinafanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara ili kuangalia utendaji kazi wake.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger