Saturday, 6 February 2016

RAIS MAGUFULI AKIWA SINGIDA KWENYE SHEREHE ZA KUZALIWA CHAMA CHA CCM

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telegrams : "CABINET"
DAR ES SALAAM
Telephone : 2116898, 2116900/6
E-mail : chief@ikulu.go.tz
E-mail : ikulu@ikulu.go.tz
Fax : 2113425/2116914/2117272
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD
11400 DAR ES SALAAM.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na wanachama wote wa CCM katika sherehe za maadhimisho ya miaka 39 ya Chama hicho zilizofanyika leo tarehe 06 Januari, 2016 katika uwanja wa Namfua, Mjini Singida.
Viongozi wengi waliohudhuria sherehe hizo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa,  Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mheshimiwa Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana pamoja na Wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, pamoja na kuwashukuru wananchi wa Singida kwa kumchagua kwa kura nyingi kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Magufuli amewaahidi kuwa atahakikisha serikali yake inatekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020 kikamilifu ili kila mtanzania anufaike na matunda ya nchi yake.
Amebainisha kuwa serikali yake imedhamiria kufanya kazi kwelikweli chini ya kauli mbiu ya "Hapa Kazi Tu" huku akionya kuwa watendaji wa serikali ambao watashindwa kutekeleza ilani ya CCM wataondoka.
Rais Magufuli ameupongeza mkoa wa Singida kwa kuchangisha fedha zilizofanikisha kutengeneza madawati 1,000 kwa ajili ya wanafunzi wa shule, na ameelekeza kuwa viongozi wa mikoa mingine waige mfano huo, vinginevyo watakuwa wamedhihirisha kuwa hawatoshi kuendelea na nyadhifa hizo.
"Haingii akilini viongozi wanakaa kwenye ofisi nzuri zenye viyoyozi lakini wanafunzi wakaa chini kwa kukosa madawati, na ikiwa hivyo, basi hicho ni kigezo tosha kuwa viongozi wa mkoa ama wilaya hiyo hawafai kuendelea na nyadhifa hizo" alisisitiza Rais Magufuli.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa awamu ya nne  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amesema kwa miaka 39 Chama hicho tawala kimefanikiwa kulinda amani, kusimamiwa usawa na uzalendo kwa watanzania na kwamba kinajivunia mafanikio hayo makubwa.
Dkt. Kikwete pia amempongeza Rais Magufuli, Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, kwa kazi nzuri wanayoifanya ambayo licha ya kukiongezea heshima Chama Cha Mapinduzi, imejenga matumaini na imani ya wananchi kwa chama chao na serikali yao.
"Naomba nikuhakikishie kuwa mimi na wana CCM wenzangu tunakuunga mkono na tunawatakia kila heri katika kutekeleza ilani ya CCM" alisema Dkt. Kikwete.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana, amesema CCM inampongeza kwa dhati Rais Magufuli kwa kazi nzuri aliyoanza kuifanya kwa kipindi cha siku 90 za tangu alipoapishwa kuwa Rais.
Ametaja baadhi ya kazi hizo kuwa ni kukabiliana na wizi wa mali ya umma, rushwa, kubana matumizi, matumizi mabaya ya madaraka na kudhibiti nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma.
"Rais Magufuli nakupongeza sana sana, unatekeleza uliyoyaahidi na wananchi wanafurahishwa sana. Endelea hivyo hivyo, mambo mazuri" Alisisitiza Ndugu Kinana

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dododma
06 Januari, 2016
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger