Tuesday 29 January 2019

BUNDI AZUA GUMZO BAADA YA KUTINGA MAPEMA BUNGENI DODOMA

Katika hali isiyo ya kawaida Ndege aina ya bundi ameonekana Bungeni akiwa juu kabisa. 

Spika wa bunge, Job Ndugai, amemshuhudia Bunge huyo laivu na kusema alipomuona alichanganyikiwa kidogo na kisha akawatoa hofu Wabunge kuwa kwa Dodoma kumuona ndege huyo mchana si tatizo isipokuwa ukimuona usiku ndio unaweza kuogopa.

Watumishi wa Bunge waliingia ndani ya jengo hilo kwa ajili ya ukaguzi na kumuona ndege huyo juu ya paa la ukumbi wa Bunge.

Ndege huyu hakutoka licha ya maofisa hao kutaka kumtoa, aliruka kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Hata hivyo, haikujulikana muda aliotoka na mahali alikoelekea lakini Spika Job Ndugai akasema ni mambo ya kawaida kwa Dodoma.

"Waheshimiwa wabunge, asubuhi tumeanza kumwona Bundi ndani ya jengo hili, lakini kwa Dodoma Bundi wa mchana hana madhara kwa hiyo ni mambo ya kawaida kabisa," amesema Ndugai.

==>>Msikilize spika hapo chini

Share:

ONYO LA RAIS MAGUFULI KWA ALIOWATEUA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewataka Wakuu wa Wilaya nchini kutotumia mamlaka yao vibaya kwa kuwaweka ndani baadhi ya watendaji wenzao ikiwa ni kinyume na sheria.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati akiwaapisha wakuu wa wilaya mbili, Mwanga pamoja na Tarime ambapo alibainisha sababu za kuwatengua waliokuwa kwenye nafasi hizo kuwa ni kutokana na kutumia vibaya mamlaka yao.

 "Mnasheria na mamlaka mlizopewa msizitumie vibaya sheria mnazo lakini msizitumie vibaya mtu anawekwa ndani halafu hamumpeleki mahakamani", alisema 
Rais Magufuli.

"Viongozi wengi wamelizungumzia hili namimi nalirudia, kuna masuala mengine hayahitaji mtu kuweka ndani yanahitaji kutoa maelekezo tu", aliongeza Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amehoji juu ya hatua mtu anayetuhumiwa kubaka watoto 11 kushindwa kukutwa na hatia na mahakama baada ya ushahidi kutojitosheleza.

Chanzo:Eatv
Share:

CLIFORD NDIMBO KAULA CAF







Cliford Mario Ndimbo.

Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF), limemteua Afisa Habari wa TFF kuwa Afisa Habari wa mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika kati ya Mamelodi Sundowns na ASEC Mimosas.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirikisho la soka nchini (TFF), Ndimbo atasimamia taarifa zote za mchezo huo utakaopigwa Ijumaa Februari 1, 2019 nchini Afrika Kusini kwenye uwanja wa Loftus Versfeld.

Mamelodi Sundowns na ASEC Mimosas zipo kundi A na mchezo huo utakuwa ni wa tatu kwa kila timu katika hatua hiyo ya makundi.

Timu hizo zote zina alama 3 baada ya kushinda mchezo mmoja na kufungwa moja. Mamelodi wapo nafasi ya tatu kwa uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa huku ASEC wakiwa katika nafasi ya 3.

Vinara wa kundi hilo ni timu ya Wydad Casablanca ambayo nayo ina alama 3 huku Lobi Stars ya Nigeria ikiwa na alama 3 katika nafasi ya 4 ya kundi hilo.

Chanzo:Eatv
Share:

MAREKANI YAISHITAKI KAMPUNI YA HUAWEI KWA TUHUMA YA WIZI

Marekani imewasilisha kesi 23 dhidi ya kampuni ya mawasiliano ya China, Huawei.

Marekani imeishtaki kampuni kubwa ya mawasiliano ya China, Huawei na afisaa mkuu wake wa fedha, Meng Wanzhou.

Mashataka hayo ni pamoja na ubadhirifu wa fedha, kupinga utekelezaji wa haki na wizi wa teknolojia.

Kesi hiyo huenda ikazua mgogoro wa kibiashara kati ya Marekani na China hali ambayo itaathiri biashara ya kampuni hiyo.

Kampuni ya Huawei imekanusha madai hayo.

Katika taarifa, Huawei imesema kuwa imeghadhabishwa na mashtaka dhidi ya yake.

Imesema kuwa haikufanya makosa yote yanayodaiwa ilitekeleza na kwamba haina ufahamu wa kosa alilotekeleza Bi Meng.

Chanzo:Bbc
Share:

WAMBURA AAMUA KUFANYA WALICHOFANYA UBELGIJI FIFA


Michael Wambura

Aliyekuwa makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura kabla ya kufungiwa maisha na TFF na kifungo hicho kuthibitishwa na FIFA, amesema hakuna chombo chenye mamlaka ya kukaidi maamuzi ya mahakama.

Wambura amesisitiza kuwa huenda FIFA hawakupewa taarifa vizuri na TFF juu ya maamuzi ya mahakama ndio maana wakaidhinisha maamuzi yako.

"Mpaka sasa kuna kesi iliyofunguliwa Ubelgiji juu ya FIFA na walikubali kuwa maamuzi ya mahakama ya ndani ya nchi husika hayaingiliwi na FIFA kwahiyo hata kwenye hili wangepewa taarifa vizuri wasingeamua hivyo wangeacha maamuzi ya mahakama'' amesema.

Aidha Wambura amesema uamuzi aliochukua ni kuijulisha kamati ya nidhamu ya FIFA kuwa taarifa ya maamuzi waliyopelekewa na TFF tayari imeshaamuliwa na Mahakama ya ndani hivyo wao hawana mamlaka.

Kwa upande mwingine Wambura ameeleza kuwa ataipa taarifa mahakama kuwa maamuzi iliyotoa ili yafuatwe wahusika wake wamegoma kutekeleza uamuzi huo.

Wambura alifunguwa na TFF kutojihusisha na soka ambapo alifungua kesi mahakama kuu ya kupinga maamuzi hayo na mahakama ilitengua uamuzi huo wa TFF lakini TFF walikwenda mbele zaidi kwa kuijulisha FIFA ambayo nayo ilibariki maamuzi ya TFF juu ya Michael Wambura.
Share:

ZIJUE ALAMA ZA BARABARANI PAMOJA NA MATUMIZI YAKE


Chanzo: Jamii Forums
Share:

MTOLEA AAPISHWA RASMI KUTUMIKIA UBUNGE TEMEKE

Mbunge wa Temeke (CCM), Abdallah Mtolea leo Jumanne Januari 29,2019 ameapishwa bungeni jijini Dodoma.

Mtolea ameapishwa baada kupita bila kupingwa kutokana na wagombea wa vyama vingine kukosa vigezo.

Alikuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CUF na alijiuzulu Novemba 15, 2018 na kujiunga CCM.

Hata hivyo, kiapo cha Mtolea leo kilikuwa tofauti na viapo vya wabunge wengine waliohamia CCM kutokea upinzani kutokana na kutokuwa na mbwembwe zilizozoeleka.

Mtolea aliingia akisindikizwa na wabunge wachache wa CCM. Mara baada ya kuapishwa na Spika, Job Ndugai alikwenda moja kwa moja kusalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Profesa Adelardus Kilangi na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenister Mhagama.

Wakati Mtolea akiapishwa wabunge wa upinzani waliokuwepo bungeni ni wa CUF upande wa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba.
Share:

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO JUMANNE 29.01.2019

Arsenal wanatizamia Gary Cahill atawasaidia kuziba mapengo kwenye safu yao ya ulinzi.

Arsenal wanataka kumsajili beki mkongwe wa Chelsea na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya England Gary Cahill, 33, ili kukabiliana na changamoto ya majeruhi inayoikabili safu yake ya ulinzi.(Mirror)

Manchester City wanampango wa kumsajili beki wa Leicester raia wa Uingereza Ben Chilwell, 22, mwishoni mwa msimu. (ESPN)

Tottenham wanapanga kumsajili kiungo raia wa Uhispania anayecheza klabu ya Valencia Carlos Soler, 22, mwishoni mwa msimu. (ESPN)

Burnley wanapiga hesabu ya kuwanunua streka Che Adams, 22, kutoka Birmingham na streka wa Tottenham Vincent Janssen, 24. (Mail)

Mchezaji nyota wa Liverpool na timu ya taifa ya Senegal Sadio Mane, 26, amesema kwa sasa Liverpool ndiyo kipaumbele chake, akionekana kupuuzia taarifa kuwa anataka kujiunga na Real Madrid. (World Soccer)


Klabu inayochecha Ligi ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1 Lille wamo mazungumzoni na klabu ya Swansea kumsajili nahodha wao raia wa Uholanzi to sign their Leroy Fer, 29. (Sky Sport)

Fer pia anawindwa na miamba ya Uturuki klabu ya Fenerbahce. (Mail)

Manchester United wamempatia kiungo raia wa Uhispania Juan Mata, 30, mkataba wa miezi 12 ili kumzuia kuondoka kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu. (Mirror)


Wolves wapo tayari kulipa pauni milioni 18 - ambayo ndiyo rekodi kubwa ya usajili - kumnunua beki raia wa Uhispania Jonny Castro Otto, 24, ambaye kwa sasa anakipiga klabuni hapo kwa mkopo akitokea Atletico Madrid. (Express & Star)

West Ham wamo kwenye mazungumzo na Celta Vigo ili kunua wachezaji wawili; streka wa Uruguay Maxi Gomez, 22, na kiungo wa Slovakia Stanislav Lobotka, 24. (Teamtalk)

Chanzo:Bbc
Share:

MAN UNITED KUUMANA NA CHELSEA MZUNGUKO WA TANO

Mabingwa watetezi wa kombe la FA, Chelsea, wataminyana na mabingwa mara 12 wa kombe hilo, Manchester United, katika mzunguko wa tano wa michuano hiyo.
Mechi ya miamba hiyo itakuwa ni marudio ya fainali ya mwaka jana mabapo Chelsea waliibuka na ushindi.

Timu ya Ligi Daraja la Pili ya Newport County wanaweza kuminyana na mabingwa wa Ligi ya Uingereza Manchester City iwapo watawang'oa Middlesbrough katika mechi yao ya marudiano.

Michezo ya raundi ya tano ya michuano ya FA itapigwa kati ya tarehe 15 na 18 ya mwezi Februari.

Chanzo:Bbc
Share:

WALIMU WASIMAMISHWA KAZI KWA KUOA WANAFUNZI WAO,WENGINE KUFELISHA MITIHANI


Peti Siyame, Mpanda 

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi, limewasimamisha kazi walimu wanne shule za msingi, kwa tuhuma za kuoa wanafunzi wao na kuwapatia ujauzito kupisha uchunguzi wa tuhuma zao.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nsimbo , Raphael Kalinga alisema kuwa walimu hao wamesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zao.

Pia, baadhi yao uhamisho wao wa kwenda kufundisha katika vituo vingine vya kazi umesitishwa, wakihofiwa kuendelea na ‘ukware’ wao huko. Majina ya walimu hao tunayo.

Kalinga ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Machimboni, alibainisha hayo katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Nsimbo kilichoketi jana.

Aidha baraza hilo la madiwani, limewashusha vyeo walimu wakuu wa shule za msingi kumi na kumvua madaraka Ofisa Elimu wa Halmshauri ya Nsimbo (Shule za Msingi), Marcus Nazi baada ya Halmashauri hiyo kuwa na matokeo mabaya ya mitihani ya taifa ya kumaliza elimu ya msingi kwa miaka miwili mfululizo.

“Wakati Nazi alipokuwa Ofisa ELimu Ufundi, Michael Nzyungu alikuwa Ofisa Elimu (Msingi) lakini kwa kipindi chake chote halmashauri haikuwahi kuwa na matokeo mabaya katika Mitihani ya Kumaliza Elimu ya Msingi .... Tulikuwa nafasi ya pili au ya tatu lakini baada ya kushika nafasi hii tumekuwa na matokeo mabaya sana ... nafasi hii imemshinda, hataendelea tena na kazi hiyo “ alibainisha.

Via Habarileo
Share:

YANGA KUCHOMOA VICHWA VITATU VYA KARIOBANGI SHARKS


Benchi la ufundi la Yanga

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera ameweka wazi kuwa anahitaji sahihi za wachezaji kadhaa kutoka klabu ya Kariobangi Sharks ili kuimarisha nafasi mbalimbali katika kikosi chake hususani eneo la ulinzi.
Zahera amesema mipango hiyo ya usajili huku akieleza kuwa klabu hiyo imejipanga vyema kuweza kupata fedha nyingi za usajili ili kuboresha kikosi chake.

''Katika klabu ya Kariobangi Sharks nawahitaji wachezaji waliovaa jezi namba 8, 7 na 17 ndiyo tunatakiwa kusajiliwa'', alisikika Zahera akieleza.

Aidha kocha huyo amesema anataka kusajili wachezaji kwenye nafasi ya mlinzi wa kushoto na kulia pamoja na mlinzi wa kati ili kukipa nguvu kikosi chake.

Yanga ilitolewa katika robo fainali ya michuano ya SportPesa na Kariobangi Sharks kwa kufungwa mabao 3-2.
Share:

MUONEKANO WA JENGO LA TAMISEMI UTAKAVYOKUWA

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) imekuja na maajabu mpya kwa kujenga Jengo la Kisasa litakalokuwa na mvuto wa kipekee katika mji mpya wa Serikali Jijini Dodoma.

Ujenzi huo unatekelezwa kwa kutumia utaratibu wa manunuzi ya moja kwa moja ‘Force Account’ na utagharimu Sh.Bilioni moja ambazo zimetolewa na Rais Dk.John Magufuli kwa kila Wizara.

Jengo hilo litachukua watumishi zaidi ya tisini pamoja na kumbi mbili za mikutano ikilinganishwa na majengo mengine yatakayochukua watumishi chini ya arobaini.


Kupitia utaratibu huo kuna kamati nne za ushindi zimeundwa ili kufanikisha ujenzi ambazo ni Kamati ya Manunuzi, Kamati ya Vifaa, Kamati ya Ujenzi, na Kamati ya Usimamizi na ufuatiliaji.


Katika kufanikisha ujenzi huo, TAMISEMI inatumia kitengo cha Ujenzi cha Chuo Kikuu Mbeya kama fundi wa ujenzi huo chini ya Wakala wa Majengo(TBA) kama mshauri.


Aidha, kamati ya ujenzi ya TAMISEMI iliyo sheheni wahandisi wake kutoka makao makuu wanasimamia kila kipande cha ujenzi huo ili kuendana sambamba na ushauri wote unaotolewa na TBA kwa lengo la kupata jengo bora zaidi.


Katika kufanikisha mapinduzi hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo alitoa maelekezo mahususi kwa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) ambayo ni Taasisi iliyo chini ya usimamizi wa Ofisi ya TAMISEMI kuhakikisha unajenga jengo la aina hiyo pia kwa kutumia fedha za ujenzi walizonazo kwasasa.


Amesema hataki kuona Taasisi hiyo inatumia fedha nyingi kwa ajili ya kupanga jengo na kwamba ifikapo Julai mwaka huu, agizo ambalo TARURA wameanza utekelezaji wake.


Kasi ya ujenzi wa jengo hilo inawapa changamoto Wakuu wa Mikoa, Wilaya, na Wakurugenzi wa Halmashauri hapa ambao wamepewa fedha za ujenzi wa ofisi lakini bado wanasuasua. Hili ni jambo la kutafakarisha kwa viongozi wote wa Mikoa, Wilaya, na Halmashauri zote nchini.

Share:

Monday 28 January 2019

ARUSHA KUPATA BANDARI KAVU

Na,Jovine Sosthy-Arusha Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Tanga imesema inasogeza huduma zake karibu na wateja wake wa Mkoa wa Arusha kwa kujenga bandari kavu maeneo ya King’ori. Akisoma taarifa ya maendeleo ya bandari ya Tanga kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha msimamizi wa bandari hiyo bwana Percival Ntetema,alisema huduma za bandari ya Tanga zimeimarika sana kwa sasa na bandari hiyo inaongoza kwa kutoa mizigo haraka kwa upande wa Afrika Mashariki. Alisema ilikuongeza ufanisi zaidi Bandari ya Tanga itashirikiana na mamlaka ya Reli Tanzania kufufua reli ya Tanga hadi…

Source

Share:

MADIWANI WAPINGANA NA MAAMUZI YA DC NJOMBE

Na.Amiri kilagalila Baraza la madiwani halmashauri ya mji wa Njombe limeazimia kuendelea kumchangisha mzazi fedha ya dawati tofauti na maagizo ya mkuu wa wilaya hiyo RUTH MSAFIRI ya kusitisha mpango huo ambao ulianza kutekelezwa na baadhi ya kata mkoani humo. Wakizungumza wakati wa kujadili hoja ya elimu katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika hii leo katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe,madiwani hao wamesema kuwa kamwe hawawezi kuludishwa nyuma na mtu mmoja katika swala la uchangiaji wa dawati kwani wazazi wenyewe wameridhia ili kuepusha watoto kukaa chini. “mwenyekiti…

Source

Share:

SUA BATCH 7B LOAN ALLOCATION FOR FIRST YEAR/TRANSFER AND CONTINUING STUDENTS WHO SECURED SPOSNSORSHIP OFFERED BY HESLB

Batch 7b loan allocation for first year/transfer and continuing students who secured sponsorship offered by HESLB in the academic year 2018/2019

VIEW THE LIST HERE

The post SUA BATCH 7B LOAN ALLOCATION FOR FIRST YEAR/TRANSFER AND CONTINUING STUDENTS WHO SECURED SPOSNSORSHIP OFFERED BY HESLB appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

COSTECH: Call for Proposals for ICGEB funded Meetings and Courses 2020

Share:

WAKUU WA MIKOA YOTE WAKABIDHIWA AWAMU YA PILI YA VITAMBULISHO VYA WAFANYABISHARA WADOGO WADOGO


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwhira vitambulisho

Wakuu wa Mikoa yote nchini wamekabidhiwa vitambulisho vya awamu ya pili vya wafanyabiashara wadogowadogo leo Jumatatu, Januari 28, 2019, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Jumla ya vitambulisho milioni moja na laki moja vimekabidhiwa kwa wakuu hao wa mikoa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, ambavyo viliasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli mwishoni mwa mwaka uliopita.

Balozi Kijazi amekabidhi vitambulisho hivyo na kuwataka wakuu wa mikoa hiyo kuhakikisha vitambulisho hivyo vinatolewa kwa wahusika na kwa wakati kwa wahusika na kuongeza kuwa tayari kuna taarifa za baadhi ya watumishi wa halmashauri ambao wanaviuza vitambulisho hivyo kwa zaidi ya bei elekezi iliyotolea na Rais.

Pia amewataka wakuu hao wa mikoa kuwachukulia hatua za kinidhamu wale wote wanaokiuka agizo hilo.

Amewataka wakuu hao wa mikoa kusimamia kikamilifu zoezi hilo la ugawaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo wadogo huku akitaja idadi ya vitambulisho ambavyo kila mkoa utakabidhiwa.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger