Saturday, 27 April 2024

KATAMBI AKABIDHI AMBULANCE NYINGINE KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA MANISPAA YA SHINYANGA

...
Na Kadama Malunde & Marco Maduhu - Shinyanga

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu amekabidhi gari maalumu la kubebea wagonjwa ‘ Ambulance’  ambalo litatumika kutoa huduma Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga.

Katambi amekabidhi Ambulance hiyo leo Jumamosi Aprili 27,2024 katika Stendi ya Magari Soko Kuu Manispaa ya Shinyanga  na kushuhudiwa na wananchi,viongozi wa Serikali pamoja na Chama Cha Mapinduzi.

Amesema hiyo ni Ambulance ya pili ambayo ameitoa katika ahadi zake, ambapo ya kwanza aliitoa February 8 Mwaka huu na leo pia amekabidhi Ambulance nyingine ili kuendelea kuboresha huduma za Afya.

"Nimekuja kwa awamu nyingine kukabidhi gari hili ‘Ambulance’ niliyopewa na Mama, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili lisaidie kuboresha huduma za afya katika Manispaa ya Shinyanga. Mimi nikiahidi natekeleza, Ambulance ambayo naikabidhi leo itatumika kutoa huduma Kituo cha Afya Kambarage na ile ilikuwa ya Kambarage kwa sababu ni ndogo itakwenda Ihapa,"amesema Katambi.

Katambi amemshukuru  Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi na kuboresha huduma za afya kwa wananchi pamoja na kutoa ajira za afya pamoja na upatikanaji wa vifaa tiba.

Katika hatua nyingine amemshukuru Rais Samia, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kwa miongozo yao na kumwezesha kufanya kazi za Serikali pamoja na kuhudumia wananchi wa Jimbo lake.

Kwa upande, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga (DMO) Dkt. Elisha Robert, ameshukuru kupata Ambulance hiyo na kwamba sasa zimefika nne katika Manispaa hiyo ambazo zitasaidia kubeba wagonjwa na kuwawahisha kupata huduma za matibabu.

Amesema ndani ya miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Manispaa ya Shinyanga zimeshajengwa zahanati mpya sita na zingine mbili zinaendelea kukamilishwa ikiwamo ya Mwamagunguli pamoja na kutoa ajira 93 za watumishi wa afya.

Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Zamda Shaban, amemshukuru Mbunge Katambi kwa kuendelea kupambania Wananchi katika suala zima la Maendeleo na sasa ameendelea kutekeleza Ahadi yake ya kuleta magari ya wagonjwa.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Makombe, ametoa wito kwamba Magari hayo ya Wagonjwa ambayo yamekabidhiwa na Mbunge kwamba wayatunze pamoja na Madereva kuyaendesha vizuri na kutosababisha ajali.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu (kushoto) akizungumza wakati akikabidhi gari maalumu la kubebea wagonjwa ‘ Ambulance’  katika Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Aprili 27,2024 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu (kushoto) akizungumza wakati akikabidhi gari maalumu la kubebea wagonjwa ‘ Ambulance’  katika Manispaa ya Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu (kushoto) akikata utepe wakati akikabidhi gari maalumu la kubebea wagonjwa ‘ Ambulance’  katika Manispaa ya Shinyanga

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akiendesha gari maalumu la kubebea wagonjwa ‘ Ambulance’ katika Manispaa ya Shinyanga
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga (DMO) Dkt. Elisha Robert akionesha vifaa vilivyomo ndani ya gari jipya la wagonjwa katika Manispaa ya Shinyanga

Gari maalumu la kubebea wagonjwa ‘ Ambulance’  lililokabidhiwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu  kwa ajili ya kutoa huduma za afya Manispaa ya Shinyanga
Gari maalumu la kubebea wagonjwa lililokabidhiwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu  kwa ajili ya kutoa huduma za afya Manispaa ya Shinyanga

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga (DMO) Dkt. Elisha Robert na watumishi wa afya wakionesha furaha baada ya kukabidhiwa gari jipya la wagonjwa 
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akizungumza wakati akikabidhi gari maalumu la kubebea wagonjwa ‘ Ambulance’  katika Manispaa ya Shinyanga

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Makombe akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya gari maalumu la kubebea wagonjwa ‘ Ambulance’  katika Manispaa ya Shinyanga
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga (DMO) Dkt. Elisha Robert akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya gari maalumu la kubebea wagonjwa ‘ Ambulance’  katika Manispaa ya Shinyanga
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Zamda Shaban akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya gari maalumu la kubebea wagonjwa ‘ Ambulance’  katika Manispaa ya Shinyanga
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Naibu Katalambula akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya gari maalumu la kubebea wagonjwa ‘ Ambulance’  katika Manispaa ya Shinyanga
Viongozi na wananchi wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya gari maalumu la kubebea wagonjwa katika Manispaa ya Shinyanga

Viongozi na wananchi wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya gari maalumu la kubebea wagonjwa katika Manispaa ya Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger