Tuesday 2 April 2024

SERIKALI KUENDELEA KUWALEA WAZALISHAJI,WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI WA NDANI

...


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa na wa Makatibu Wakuu unaojumuisha Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu Mwamba, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu wakiwa na Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Bw. Rashid Mchatta walipotembelea Kiwanda cha Kiwanda cha Kairuki Pharmaceutical Industry Limited kilichopo Kibaha Mkoa wa Pwani Machi 30,2024 kujionea shughuli za uzalishaji na kutatua changamoto.

 ............... 

Serikali itaendelea kuwalea wazalishaji wawekezaji na wazalishaji wa ndani ya nchi ili waweze kukuza mitaji yao na kuchangia katika maendeleo ya ya Taifa kwa ujumla. 

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah, wakati wa ziara yake kwenye Kiwanda cha Kairuki Pharmaceutical Industry Limited kilichopo Kibaha mkoani Pwani tarehe 30 Machi 2024. 

Akiongoza ujumbe wa Makatibu Wakuu wakiwemo Dkt. Natu Mwamba (Wizara ya Fedha), Dkt. John Jingu (Wizara ya Afya), na Bw. Rashid Mchatta (Katibu Tawala Mkoa wa Pwani), Dkt. Abdallah alieleza kuwa lengo la ziara hiyo lilikuwa kujionea shughuli za uzalishaji, kusikiliza changamoto zinazokikabili Kiwanda hicho na kutafuta suluhisho. 

Dkt Abdallah pia alibainisha kuwa Ziara hii inaashiria dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuimarisha sekta ya viwanda nchini kwa kuwaunga mkono wawekezaji wa ndani na kuwawezesha kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya uchumi wa Taifa.

Dkt. Abdallah akiwa na ujumbe huo alikipongeza Kiwanda hicho kwa utendaji kazi mzuri na kuahidi ushirikiano kutoka kwa wizara husika katika kutatua changamoto zilizopo ili kuwezesha kiwanda hicho kufanya kazi kwa ufanisi Vilevile. 

Alibainisha kuwa Kiwanda hicho kinachotoa ajira za moja kwa moja 200 na zisizo za moja kwa moja 300 ni moja ya Kiwanda cha kimkakati kinacholzalisha dawa za maji tiba (Fluid Therapy) mbalimbali Nchini ili kupunguza utegemezi wa kuagiza dawa hizo nje ya nchi. 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda hicho Dkt Muganyizi Kairuki akitoa taarifa kwa ujumbe huo amesema Kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha chupa za maji tiba milioni 50 kwa mwaka ambapo asilimia 60 huuzwa nchini wakati asilimia 40 huuzwa Nchi za nje zikiwemo Rwanda, Comorro, Malawi, Zambia, Namibia, Congo, Mozambique na Yemen


 Vilevile ametaja baadhi ya Dawa zilizosajiliwa kuzalishwa kiwandani hapo kuwa ni pamoja na "Sodium Chloride (0.9%w/v), Compound Ringer Lactate, Dextrose (5%w/v) &Sodium Chloride(0.9%w/v), Dextrose (5%w/v ) na Dextrose(10%w/v). Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa na wa Makatibu Wakuu unaojumuisha Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu Mwamba, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu wakiwa na Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Bw. Rashid Mchatta walipotembelea Kiwanda cha Kiwanda cha Kairuki Pharmaceutical Industry Limited kilichopo Kibaha Mkoa wa Pwani Machi 30,2024 kujionea shughuli za uzalishaji na kutatua changamoto.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger