Tuesday, 22 January 2019

RAIS MAGUFULI AMTAKA BITEKO ASIANGALIE SURA YA MTU.. " UTAZIKWA PEKE YAKO"


RAIS John Magufuli amemtaka Waziri wa Madini, Dotto Boteko atekeleze majukumu yake bila kujali sura ya mtu kwa kuwa kaburini atakwenda peke yake.

Amesema, hasiti kumfukuza Waziri wa Madini hata kama ameiongoza Wizara hiyo kwa wiki moja.

Amewataka viongozi wa Wizara hiyo wachukue hatua, wawahamishe wataalamu wizarani na atashangaa kama hilo halitafanyika.

Ametoa maagizo hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anafungua mkutano wa mashaurino wa wafanyabiashara na wadau wa sekta ya madini.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuufunga kesho.

Rais Magufuli amemtaka Waziri wa Madini Dotto Biteko awe mkali, na kwamba, aliyepita, Angellah Kairuki hakuwa mkali ndiyo maana kampeleka akapumzike Ofisi ya Waziri Mkuu.

Kairuki ni Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji.

Rais Magufuli amemuagiza Waziri Biteko, Naibu wake, Stanslaus Nyongo na Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa Amos Msanjila hiyo ndani ya mwezi mmoja wawe wameweka kamera kwenye ukuta wa Mirerani na wasipofanya hivyo wajiandae kuondoka.

Via Habarileo
Share:

WAZIRI AGOMA KUTUMBULIWA NA RAIS MAGUFULI

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema hayupo tayari kutimuliwa na Rais John Magufuli kwa kushindwa kupeleka huduma za maji kwa wananchi.

Kauli ya Aweso imetokana na kusuasua kwa utekelezaji wa miradi ya maji katika wilayani Kisarawe mkoani Pwani licha ya bajeti iliyopo.

Akizungumza leo Jumanne Januari 22, 2019 wakati wa ziara ya kikazi katika wilaya hiyo, Aweso amesema Rais Magufuli alipomteua alimpa jukumu la kuhakikisha maji safi na salama yanawafikia wananchi wote.

Kauli hiyo ya Aweso imetokana na kusuasua kwa miradi ya maji wilayani humo huku mkuu wa wilaya hiyo, Jokate Mwegelo akisema imeshindwa kuendelea kwa kukosa huduma ya maji.

"Tulipoteuliwa katika nafasi hizi Rais alisema anatupa wizara hii ili wananchi wapate maji na wasipopata basi atatumbua na mimi sipo tayari kutumbuliwa," amesema Aweso.


Na Cledo Michael, Mwananchi
Share:

KKKT NJOMBE SASA RUKSA KUUZA VIWANJA, ASKOFU MENGELE ATUMA SALAMU KWA WALIOKWAMISHA ZOEZI

Na Amiri kilagalila Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania kanda ya nyanda za juu kusini limejipanga kuendelea na zoezi la uuzaji wa viwanja vinavyomilikiwa na kanisa hilo mkoani Njombe kutokana na maagizo ya kusitishwa uuzaji wa maeneo hayo lilitolewa na waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi alipokuwa mkoani Njombe siku chache zilizopita Askofu wa kanisa la KKKT Dayosisi ya kusini Njombe Isaya Japhet Mengere amesema kuwa serikali kupitia wizara ya ardhi nyumba na makazi imeruhusu zoezi la uuzaji viwanja katika eneo linalojengwa chuo kikuu mjini Njombe…

Source

Share:

KK SHARKS WAICHAPA YANGA 3 - 2

Mlinda  mlango namba moja wa Yanga, Klaus Kindoki amekubali kuokota mipira mara mbili nyuma ya nyavu katika mchezo wa michuano ya SportPesa Cup ambao umechezwa Uwanja wa Taifa.

Yanga amecheza na KK Sharks ya Kenya na Kindoki amegeuka mara tatu baada ya kuanza mapema dakika ya 12 kuokota mpira nyuma ya wavu na kufanya hivyo dakika ya 36.

KK Sharks wamerejea kipindi cha pili wakiwa wanaongoza kwa mabao 2-0 ambayo wameyapata katika kipindi cha kwanza baada ya kushambulia sana lango la Yanga.

Kipindi cha pili dakika ya 87 Yanga wakapata bao la kufutia machozi kupitia kwa Amiss Tambwe na dakika ya 90 bao la pili kupitia kwa Makambo.

KK Sharks nao wakafanikiwa kufunga bao la 3 dakika ya 90.


Share:

NDEGE YAPOTEA ANGANI..YUMO MSHAMBULIAJI MPYA WA CARDIFF CITY


Mchezaji Sala ambaye alikuwa kwenye ndege hiyo.

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Cardiff City Emiliano Sala, amepotea angani kwenye ndege binafsi jana jumatatu jioni wakati anatoka mjini Nantes, Ufaransa kuelekea Cardiff, Wales.

Mamlaka ya anga ya Ufaransa imethibitisha ndege hiyo kupotea ambapo muargentina huyo mwenye miaka 28 alikuwepo pamoja na mtu mwingine wa pili.

Sala alisajiliwa kwa ada ya rekodi ya klabu hiyo ya pauni milioni 15 siku ya Jumamosi na alikuwa ni miongoni mwa watu wawili waliokuwepo kwenye ndege hiyo iliyopotea.

Baada ya kusaini mkataba siku ya Jumamosi, Sala alirejea nchini Ufaransa kuwaaga wachezaji wa timu yake ya zamani ya Nantes, na baadaye kuweka picha akiwa na wachezaji hao katika Instagram akiandika “ Kwa heri ya mwisho “ kabla ya kupanda ndege kurejea Wales.

Afisa anayehusika katika kuitafuta ndege hiyo John Fitzgerald anasema kuwa hatarajii kumkuta mtu yoyote akiwa hai.

“Kuna bahati ya asilimia 5 tu ya kuwapata Sala na rubani, “alisema Fitzgerald.‘ Maji ni ya baridi sana kwa sasa , kwa hiyo kama kuna ambaye amepona kwenye maji , ni baridi sana , ni saa moja tu unaweza kuwa mzima katika kipindi hiki cha mwaka‘ .

Familia ya mchezaji huyo ipo nchini Argentina na baba wa mchezaji huyo Horacio amesema alijisikia vibaya sana baada ya kupata taarifa za kupotea kwa mwanae.
Share:

OLE GUNNA SOLSKJAER NA UNAI EMERY KUKUTANA IJUMAA HII EMIRATES FA CUP


Raundi ya 4 ya michuano ya Emirates FA CUP, kuanza kupigwa Ijumaa hii ambapo kwa mara ya kwanza Ole Gunna Solskjaer na Unai Emery wanakutana, ni katika pambano la FA Emirates Cup, Je ni kocha gani kuanza kuandika rekodi ya ushindi dhidi ya mwenzie?

Share:

AZAM FC NA SIMBA FEBRUARI 22 NA YANGA APRILI 29 UWANJA WA TAIFA

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imepanga ratiba za mechi za viporo za Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, itakazocheza dhidi ya Simba na Yanga zilizotakiwa kufanyikwa kwenye raundi ya kwanza.

Ratiba hiyo mpya inaonyesha kuwa Azam FC itacheza mechi ya kwanza ya ligi dhidi ya Simba msimu huu, Februari 22 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku ile na Yanga ikipigwa Aprili 29 mwaka huu.

Mechi nyingine mbili za viporo za Azam FC, dhidi ya Mbeya City na Ndanda, ilizotakiwa kucheza kwenye raundi mbili za awali za mzunguko wa pili wa ligi hiyo, itakipiga na City Aprili 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa Sokoine, kabla ya kusafiri hadi mkoani Mtwara kumenyana na Ndanda Aprili 18.

Katika mabadiliko hayo ya ratiba inaonyesha kuwa, msimu wa ligi utafungwa Mei 26 mwaka huu kwa mechi zote kupigwa huku Azam FC ikitarajiwa kufunga pazia hilo kwa kumenyana na Yanga, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wiki hii Azam FC inatarajia kukamilisha raundi ya 24 ya ligi kwa kucheza na Biashara United, mchezo utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex Ijumaa hii saa 1.00 usiku, kabla ya kuhamishia nguvu kwenye Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) ikitarajia kukipiga na Pamba kwenye dimba hilo Januari 28 mwaka huu saa 1.00 usiku.

Azam FC hadi sasa imeonekana kufanya vizuri kwenye msimu huu wa ligi, ikiwa ni miongoni mwa timu zinazopigana vikumbo kuwania taji hadi sasa ikiwa nafasi ya pili ikiwa imejikusanyia pointi 44 ikizidiwa pointi tisa na Yanga iliyo kileleni, lakini matajiri hao wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Share:

HATIMAYE MAKAMANDA WALIOTENGULIWA NA KANGI LUGOLA WAONDOLEWA



Share:

SHUWASA YATOA KALENDA ZA 2019 KWA WAANDISHI WA HABARI MANISPAA YA SHINYANGA

Ofisa Mahusiano ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA), Nsianel Gelard ( wa kwanza kulia)  akimkabidhi Kalenda za mwaka 2019 Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC),Kadama Malunde kwa ajili ya Waandishi wa Habari waliopo katika Manispaa ya Shinyanga katika ofisi ya SPC leo Jumanne Januari 22,2019. Picha na Malaki Philipo - Malunde1 blog
Kulia ni Ofisa Mahusiano ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA), Nsianel Gelard akimkabidhi Kalenda za mwaka 2019 Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC),Kadama Malunde
Zoezi la makabidhiano ya kalenda likiendelea. Wa kwanza kulia ni Ibrahim  Mwita kutoka SHUWASA,Wa pili kutoka kushoto ni Mweka Hazina wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC), Stella Ibengwe.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC), Kadama Malunde akiwa ofisini baada ya kupokea kalenda kutoka SHUWASA
Share:

KAKOBE: TANZANIA ILIKUWA IKIISHI NA LAANA

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe amedai Tanzania ya zamani ilikuwa ikiishi kama nchi yenye laana kutokana na baadhi ya rasilimali zake kutumika zaidi na wageni na kushindwa kuwafaidisha watanzania wenyewe.

Askofu Kakobe ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam kwenye mkutano wa wadau wa uchimbaji na wafanyabiashara ambapo walizungumza na Rais John Pombe Mgufuli ili kuhakikisha sekta hiyo inainua uchumi wa Tanzania.

 “lakini ni jambo la kushukuru kwa sababu Mungu amemuinua shujaa Rais Magufuli ambaye amekataa kwamba tuachiwe mashimo na urithi wetu wachukue mataifa mengine na suala hili linahitaji ushujaa sana,”  Askofu Kakobe alisema,.

 “hata Biblia inasema tutangulize yaliyo mema hata kama una hasira naye, hata Yesu Kristo alipokuwa anatoa ujumbe kwa makanisa saba alikuwa anaanza kupongeza mazuri hata kabla ya kuinua jambo lolote la kupinga, atakayekuwa anapinga atakuwa ni mkorofi na hata ukiwa na hoja itakuwa ngumu kusikilizwa,ameongeza Askofu Kakobe.

“Mimi nafikiri unapoanza kupambana na suala hili, uanze kufanyia kazi kwanza fikira za mtu. Kadiri tunapozidi kutamka vitu vizuri ndiyo tunazidi kuvichochea,” aliongeza Kakobe.

Chanzo:Eatv
Share:

WATOTO WA MAZINGIRA MAGUMU WAIANGUKIA SERIKALI

Na. Danson Kaijage-Dodoma. WATOTO wanaolelewa kwenye vituo jijini Dodoma wameiomba serikali kudhibiti taasisi,mashirika na watu binafsi wanaojihusisha na utapeli wa kivuli cha watoto yatima na kujipatia mamilioni ya fedha na misaada mbalimbali ambayo haiwafikii walengwa. Ombi hilo lilitolewa na watoto wanaolelewa katika kituo cha Shirika la Malezi Endelevu (SHIME) jijini Dodoma Raheli Rafael na Moses Tobias kwa niaba ya wezao wakati walipokuwa wakipokea misaada mbalimbali iliyotolewa na wanavyuo kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Wakizungumza baada ya kupatiwa misaada hiyo iliyotolewa na wanavyuo kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) watoto…

Source

Share:

MAKONDA AMTAKA SPIKA NDUGAI AMPELEKE TUNDU LISSU MILEMBE.

Na,Mwandishi wetu. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewaomba watanzania kumsamehe Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antiphas Lissu kwa kauli anazozitoa huko nje ya nchi. Makonda ametoa kauli hiyo leo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, katika Mkutano wa Wachimbaji, Wafanyabiashara na Wadau wa sekta ya madini nchini. Makonda amesema kwamba amegundua kwamba kauli za Lissu zinatokana na kwamba bado hajapona vizuri kichwani kutokana na yeye mwenyewe kukiri wakati alipokuwa akimaliza mahojiano katika kipindi cha ‘Hard Talk’ kilichofanyika jana na kituo…

Source

Share:

SIMBA KUSAJILI WACHEZAJI WAWILI KUTOKA MAGHARIBI

Mchezaji Lamine Moro kutoka Ghana.

Taarifa ya klabu hiyo leo imeeleza kuwa wachezaji walioletwa ni wa eneo la ulinzi na ushambuliaji ambao wanatoka mataifa ya Ghana na Togo na watasajiliwa endapo kocha Patrick Aussems ataridhishwa na kiwango chao.

''Wachezaji Lamine Moro kutoka Ghana (beki) na Hunlede Kissimbo Ayi-Abel kutoka Togo (mshambuliaji) wamejiunga na timu yetu kwa majaribio'', imeeleza taarifa hiyo.

Aidha taarifa imefafanua kuwa iwapo Kocha Mkuu Patrick Aussems ataona wanafaa kuwatumia katika mashindano yanayoikabili timu hiyo watasajiliwa.

Tetesi zinaeleza kuwa endapo nyota hao watafuzu italazimika wachezaji wawili wa kimataifa wawili waachwe huku Pascal Wawa na Juuko Murushid, tetesi zinaeleza kuwa wanaweza kuachwa katika eneo la ulinzi.

Simba tayari ina wachezaji 10 wa kimataifa ambao ndio wanatambulika kwa mujibu wa kanuni za TFF hivyo hawaruhusiwi kuongeza.

Chanzo:Eatv
Share:

WAUZA MADINI WALIVYOIBA BENKI KUU

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Bernard Y. Kibesse.

Dkt. Kibesse ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam, katika Mkutano wa wachimbaji, Wafanyabiashara na Wadau wa sekta ya madini nchini.

Awali kabla ya kujibu swali la Rais Magufuli ambaye aliuliza BOT imejipangaje licha ya kuwa hapo nyuma ilikuwa ikishirikiana na wauzaji wanaoibia serikali.

Dkt. Kibese amesema kwamba Benki Kuu haina tatizo na kununua dhahabu, hapo awali mpaka mwaka 1994 BoT ilikuwa ikinunua dhahabu, "taifa lenye watu wasio waaminifu, haliwezi kuwa Taifa endelevu, kilichotukuta tuliuziwa dhahabu feki tukaamua kusimamisha ununuzi".

Ameongeza kuwa, "Tunafahamu kuwa 'Reserve' za Benki Kuu nyingi duniani zinakuwa na hazina za dola na dhahabu, nasi tunaweza lakini tupo tayari kuanza kununua tena. Tunaelewa Benki Kuu nyingi zinakuwa na hazina ya dhahabu".

Chanzo:Eatv
Share:

MAGUFULI AMTAKA WAZIRI ALIYEKAIDI AGIZO LAKE AJIANDAE KUACHIA OFISI

Rais John Pombe Magufuli amemtaka Waziri wa Madini, Dotto Biteko ajiandae kuachia ofisi yeye pamoja na Naibu Waziri wake endapo atashindwa kufunga kamera katika ukuta wa madini.

Rais amesema hayo leo wakati akihutubia mkutano wa Wachimbaji, Wafanyabiashara na Wadau wa sekta ya madini nchini.

"Niliagiza kufungwe Kamera katika ukuta wa Mererani lakini mpaka sasa hazijafungwa, ndio tatizo la Mawaziri wa Tanzania unatoa maagizo hawasikilizi" amesema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli ameongeza kwamba, "Nakuagiza tena Waziri Biteko, kafunge kamera ndani ya mwezi huu maana usipofanya hivyo ujiandae kuondoka na Naibu wako na makatibu wako, yaani hadi niondoke na nyie nimewamaliza".

Pamoja na hayo Rais ametaka Waziri Biteko kuwa mkali katika Wizara hiyo, "Nakuagiza uwe mkali, aliyekuwa Waziri mwenzako hakuwa mkali ndiyo maana nikaamua aende akapumzike ofisi ya Waziri Mkuu".
Share:

CHRISS BROWN AKAMATWA NA POLISI KWA UBAKAJI


Msanii wa muziki nchini Marekani, Chriss Brown na wenzake wawili wamekamatwa na polisi wakituhumiwa kwa makosa ya ubakaji.

Tukio hilo limetokea mchana huu Jijini Paris, Ufaransa, baada ya kuwa kwenye uchunguzi wa tuhuma za kudaiwa kumbaka binti wa miaka 24 ambaye alikutana naye katika maeneo ya starehe ya usiku, Januari 15.

Mwanamke huyo alimfungulia mashtaka Chriss Brown akilalamika kumfanyia kitendo hicho cha kikatili, alipomualika chumbani kwake akiwa na mwanamke mwenzake, lakini alipokuwa akitoa maelezo yake alienda mwenyewe chumbani na kukutwa na tukio hilo.

Pia mwanamke huyo aliieleza polisi ya Ufaransa kuwa hata walinzi wa msanii huyo mwenye kipaji cha aina yake walimnyanyasa, na ndipo polisi ikaanzisha uchunguzi juu ya tuhuma hizo.

Mpaka sasa Chriss Brown hajatoa kauli yoyote juu ya tuhuma hizo, na bado yuko nchini Ufaransa ambako alikuwa na ziara.
Share:

GWAJIMA AMPA USHAURI MZITO RAIS MAGUFULI

Mchungaji wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amemshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuunda timu ya watu wenye uzoefu mkubwa na wanaoijua siasa ya madini kimataifa, ili kuweza kupata soko kubwa zaidi.

Mch. Gwajima ametoa ushauri huo alipokuwa akizungumza mbele ya Rais Magufuli kwenye mkutano mkuu wa kisekta wa wizara ya madini.

Kwenye ushauri huo Askofu Gwajima ambaye alianza kwa kumsifu Rais Magufuli, amesema kwamba ni vyema akaunda timu ya watu wenye 'exposure' kwenye siasa ya madini, kwani itasaidia kuweza kupenya kwenye soko la kimataifa.

“ Leo umekuwa kama Nabii, nitoe ushauri kwa Mh. Rais, si kweli kama hakuna soko la madini, dhahabu yenyewe ni fedha, isipokuwa nashauri kama ikikupendeza, uwe na watu wenye exposure kwenye siasa za madini kimataifa, sisi kwa asili tuna dhahabu, huwezi kutuambia tumechukua dhahabu ya wengine tuthibitishe ni za kwetu, hizo ni siasa tu za masoko, unaweza ukaunda watu wenye exposure ambao wanaweza kufikia masoko mbali mbali duniani”, amesema Askofu Gwajima.

Sambamba na hilo Mchungaji Gwajima ameendelea kueleza kwamba madini tuliyonayo ni mengi na yanakosa soko kutokana na sababu mbali mbali, na iwapo yangelipiwa ushuru yasingezagaa, hivyo kama ambavyo aliwahi kukutana nayo watu wakiyauza kwenye bakuli barabarani.

"Nilipita Mwadui nikashangaa, wakaniuliza tukuletee almasi kwa utani, ndani ya saa moja watu walileta almasi imejaa bakuli haina watu wa kununua, wametoka nazo ndani ya nyumba zao, hizo kama zingelipiwa ushuru nchi yetu ingekuwa mahali pazuri sana”, amesema Gwajima

Hii leo Rais Magufuli amefanya Mkutano na wadau wa Sekta ya Madini, ambao pia uliwakutanisha na wadau na wafanyabiashara ya madini yaliyopo nchini.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger