Monday, 15 December 2025

KIKUNDI CHA WAMANDA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA MAONO YAKE

...


Kikundi cha Akinamama wanaonufaika na Mikopo ya asilimia kumi ya Halmashauri cha Wamanda kilichopo Nzega Mkoani Tabora wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa usimamizi na maboresho makubwa ya mfumo wa Mikopo hiyo, wakisema imewasaidia kiuchumi na kuwaongezea kipato kwa asilimia kubwa.

Bi. Stellah William, Kwa niaba ya wanakikundi wenzake amesema kupitia kipato wanachokipata sasa kupitia kikundi hicho, ameweza kusomesha watoto, kuendesha maisha pamoja na kumpa ujasiri mkubwa wa kuweza kutafuta fedha na kujiendeleza kiuchumi.

"Kwakweli kikundi hiki kimeninufaisha kwenye kusomesha watoto na wajukuu wangu, naendelea pia kunufaika na mambo mengi sana na zaidi kimenifanya niwe jasiri wa kutafuta fedha nikiwa peke yangu."

Nimpongeze pia Mama Samia kwa kuwa na maono yake ya kuona kuwa hata Kijijini kuna watu wanahitaji msaada wake na nimuombe Mama Samia asituchoke, tunamuhitaji sana na atuangalie kwa macho yake yote sisi akinamama wa Vijijini." Amesisitiza Bi. Stellah William.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger