Na Mwandishi wetu- Malunde 1 blog
Mdau wa maendeleo, Mhandisi James Jumbe, amewasha mishumaa ya furaha na matumaini kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Shinyanga Society Orphanage Centre baada ya kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Sikukuu ya Krismasi leo.
Msaada huo uliolenga kuongeza furaha kwa watoto hao katika Manispaa ya Shinyanga, umekabidhiwa kwa niaba yake na Ndg. Masuka Jumbe, ambaye amesisitiza umuhimu wa jamii kuyakumbuka na kuyajali makundi maalum, hasa katika msimu huu wa upendo na kutoa.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Masuka Jumbe ameeleza kuwa Mhandisi Jumbe ameona ni vyema kusherehekea siku hii ya leo kwa vitendo kwa kugusa maisha ya watoto hao.
"Katika kusherehekea Sikukuu hii ya Krismasi, Mhandisi ameona asiyaache nyuma makundi maalum. Tumefika hapa ili kusherehekea nao kwa pamoja, kwani ni muhimu kuwafariji na kuwapatia mahitaji yanayotakiwa," amesema Masuka Jumbe.
Aidha, Masuka ameongeza kuwa kitendo hicho si cha mara moja, bali ni mwendelezo wa moyo wa kutoa wa Mhandisi Jumbe kwa jamii ya Shinyanga.
"Hii siyo mara ya kwanza; mwaka uliopita tulileta mahitaji, na safari hii pia siyo ya mwisho. Tutaendelea kutoa misaada na kuwatia moyo hawa watoto ili wajione kuwa ni sehemu ya jamii yetu", amesema.










0 comments:
Post a Comment