Saturday, 13 December 2025

E- MREJESHO KUKUZA UWAJIBIKAJI KWA WATUMISHI WA UMMA

...

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Wizara hiyo imefanya maboresho mbalimbali ya mifumo yake ikiwemo mfumo wa e- mrejesho, ili kutoa fursa zaidi kwa wananchi wa pembezoni kutoa maoni, malalamiko na pongezi kuhusu huduma zinazotolewa na serikali na Taasisi zake.

Mhe. Ridhiwani amebainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar Es Salaam, akisema mfumo huo unapatikana kwenye simu za mkononi kupitia nambari *152*00#, ukiwa na module ya sema na Kiongozi, sehemu inayomruhusu mwananchi kutoa maoni kwa Waziri, Mkuu wa Mkoa ama Kiongozi mwingine, akisema mfumo huo utakusanya maoni na kisha kuchakatwa na kufanyiwa kazi.

"Mfumo huu wa e- mrejesho ni kiunganishi cha moja kwa moja cha mwananchi na Kiongozi na hii itatusaidia pale tunapojadili namna ya kuboresha mifumo ya utumishi wa umma na ni mfumo wa kweli huu, hata kama kuna Kiongozi hatojibu sisi tutasimamia kuhakikisha majibu yanapatikana." Amesema Mhe. Ridhiwani.

Aidha Mhe. Ridhiwani amehimiza wananchi kuutumia mfumo huo katika kutoa maoni yao, akisisitiza kuwa maboresho hayo yanaenda sambamba na utengenezaji wa Aplikesheni itakayowezesha wananchi kutoa mrejesho wa haraka na wa uwazi ili kuimarisha uwajibikaji wa watumishi wa serikali.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger