Viongozi wakipiga makofi wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign”
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amezindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” inayotokana na azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kwamba msaada wa kisheria unatolewa kwa wananchi wote ili kupata haki, usawa, amani na maendeleo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo leo Jumapili Juni 11,2023 katika uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga, Mndeme amesema lengo kuu la kampeni hiyo ni kulinda na kukuza upatikanaji wa haki kwa wote kupitia huduma ya msaada wa kisheria nchini.
“Kampeni hii ni utekelezaji wa Katiba yetu. Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 imetambua umuhimu wa upatikanaji haki kwa wananchi kwa kuwa Ibara ya 231(k) ya Ilani imetuelekeza “kuimarisha huduma za msaada wa kisheria hususan kwa wanawake na Watoto katika maeneo yote”, amesema.
Amesema Kampeni hiyo imekuja katika muda muafaka kwani wananchi wa Shinyanga wana uhitaji mkubwa wa msaada wa kisheria katika nyanja tofauti hususan kuelewa haki zao, wajibu wao, namna ya kutatua migogoro ya ardhi, ndoa, masuala ya mirathi, wosia na utawala bora.
“Tumejipanga kikamilifu katika kuhakakisha kuwa wananchi wa Tanzania wananufaika na Mama Samia Legal Aid Campaign. Utekelezaji wa kampeni hii ulifanyika jijini Dodoma tarehe 27 Aprili, 2023, vilevile ilizinduliwa Zanzibar tarehe 9 Mei, 2023. Na awamu hii Kampeni hii imefika Shinyanga, na kupitia huduma hii, msaada wa kisheria unatolewa bure katika Halmashauri zote sita kuanzia tarehe 11 Juni, 2023. Wananchi wote mnaalikwa kushiriki na kupata huduma zinazotolewa”,amesema Mkuu huyo wa Mkoa wa Shinyanga.
Amefafanua kuwa Kampeni hiyo yenye kauli mbiu ‘Msaada wa Kisheria kwa haki, usawa, amani na maendeleo’ inalenga kuongeza uelewa wa kisheria na haki za binadamu kwa jamii hususan haki za wanawake na watoto,Kuimarisha huduma ya ushauri wa kisheria kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia na kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu elimu ya sheria kwa umma, masuala ya haki na wajibu na misingi ya utawala bora.
Madhumuni mengine ni Usimamizi wa mirathi na urithi, sheria ya ardhi na haki ya kumiliki mali na Utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala, hususani kwa viongozi wa Serikali za Mitaa, Watendaji wa Kata, Vijiji, na Wajumbe wa Mabaraza ya ardhi, Wazee wa kimila na Wazee maarufu na Viongozi wa dini.
“Ninatoa wito kwamba sisi sote tushikamane katika kumuunga mkono Kiongozi wetu, Mama yetu, Mlezi wetu na Mtetezi wa Wananchi hususan wanyonge Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania katika kuondoa kadhia na viashiria vyote vya kuminya upatikanaji wa haki hususani ukatili wa kijinsia kwa Wanawake na Watoto ambayo ndiyo changamoto kubwa ya Mkoa wa Shinyanga”,amesema Mndeme.
Ili kuchochea upatikanaji haki na kwa wakati, Mkuu huyo wa Mkoa ametoa wito kwa Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) kushughulikia kesi zote za ndoa, mimba za utotoni na ubakaji ambazo zimekaa muda mrefu katika upepelezi bila kushughulikiwa kwa kuhakikisha watuhumiwa wanapatikana na wanashughulikiwa ili kuondoa changamoto ya kutoroka kwa watuhumiwa pindi wanapopewa dhamana ama wanaposikia wanatafutwa na Jeshi la Polisi.
“Kampeni hii inatukumbusha uwajibikaji na usimamizi wa maamuzi yenye kuleta haki, hivyo niwakumbushe watumishi wote kutojihusishwa na masuala ya rushwa inayopelekea kudhorotesha upatikanaji haki. Katika kutekeleza Kampeni kwa kipindi cha miaka mitatu, tunamuahidi Mheshimiwa Rais tutasimamia maadili kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa haki kwa usawa”,ameongeza Mndeme.
Wadau kutoka mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria na wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
“Napenda kutumia fursa hii kuwatambua na kuwashukuru Wadau wa Maendeleo wa Mkoa wa Shinyanga waliounga mkono Serikali katika kufanikisha shughuli ya Uzinduzi wa Kampeni ambao ni Shirika la Umoja wa Mataifa la UNFPA, Barrick Gold mine, NACOPHA, ICS, LSF, WILDAF, TCRS, World Vision, LULEKIA Company,Jambo Group of Companies, Taasisi zote za Umma, Makampuni ya Mitandao ya simu ( HALOTEL, VODACOM na AIRTEL) na Vyombo vyetu vya habari. Tunawashuruku kwa kutambua umuhimu wa shughuli hii kwa watanzania husuan ambao wapo kwenye maeneo ambayo kawaida hawafikiwi na huduma hizi”,ameongeza Mndeme.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul amempongeza Rais Samia kwa namna anavyoendelea kugusa Maisha ya watanzania kila sekta ikiwa ni pamoja na kutoa fedha kila sekta kwa ajili ya maendeleo.
“Mhe. Rais Samia anaboresha mfumo wa haki jinai na sasa ameleta msaada wa kisheria bure kwa Watanzania. Naagiza wakurugenzi na wakuu wa wilaya mkasimamie kampeni hii. Niombe kwenu wanashinyanga nendeni mkahamasishe wananchi kwenye maeneo yenu waje wapate msaada wa kisheria. Naomba wananchi hata kama bado haujapata tatizo njoo upate elimu ili uweze kusaidia watu wengine”,amesema Gekul.
“Viongozi wa ngazi zote kuanzia ngazi za vitongoji hadi mkoa muwe na wivu na jambo hili kwani litatatua migogoro mingi katika jamii, elimu itatolewa na wananchi watatatua migogoro yao. Mioyo ya wananchi itapata amani kwani watapata msaada wa kisheria kwani Kampeni hii inagusa masuala ya wosia,ardhi,ndoa, mirathi ambayo yanagusa wananchi wetu", ameongeza Gekul.
Kaimu Mwenyekiti wa Uratibu wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria “Mama Samia Legal Aid Campaign”, John Shija.
Naye Kaimu Mwenyekiti wa Uratibu wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria “Mama Samia Legal Aid Campaign”, John Shija ambaye ni Mwenyekiti wa Huduma za msaada wa Kisheria Mkoa wa Shinyanga ameitaja migogoro inayoongoza mkoani Shinyanga kuwa ni ardhi, ndoa, kazi na matunzo ya watoto hivyo kampeni hiyo itakuwa sehemu ya suluhisho la kumaliza migogoro.
Kwa upande wake, Meneja Rasilimali na Mawasiliano kutoka Legal Services Facility (LSF), Jane Matinde ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Shinyanga kwa maandalizi mazuri kwa ajili ya kufanikisha Kampeni hiyo na kwamba kampeni hiyo itasaidia kusuluhisha migogoro mbalimbali ndani ya jamii na kuongeza uelewa kuhusu haki za binadamu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mary Makondo amesema Tanzania imeendelea kupiga hatua kubwa katika utekelezaji wa utawala wa sheria na kuheshimu haki za binadamu na haki za watu na katika kuhakikisha hali hiyo inakuwa endelevu, Serikali kwa kushirikiana na wadau wetu imekuwa ikisimamia vizuri eneo la utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria na uzingatiwaji wa haki za binadamu na watu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mary Makondo na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa amesema CCM ina ofisi katika kata zote hivyo kuahidi kuwa wapo tayari ofisi hizo zitumike kutoa huduma za msaada wa kisheria endapo itahitajika.
Nao wabunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba na Dkt. Christina Mzava wamemshukuru Mhe. Rais Samia kwa kukubali jina lake litumike katika Kampeni hiyo huku wakisema ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ambapo itasaidia kupunguza migogoro mbalimbali katika jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (wa pili kulia) akizindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” leo Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga. Wa kwanza Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mary Makondo na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul. Kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (wa pili kulia) akizindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” leo Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mary Makondo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.

Kaimu Mwenyekiti wa Uratibu wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria “Mama Samia Legal Aid Campaign”, John Shija ambaye ni Mwenyekiti wa Huduma za msaada wa Kisheria Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Meneja Rasilimali na Mawasiliano kutoka Legal Services Facility (LSF), Jane Matinde akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Dkt. Christina Mzava akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Donald Magesa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Kikundi cha Shinyanga Arts kikitoa burudani wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wakicheza wakati Kikundi cha Shinyanga Arts kikitoa burudani kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Viongozi na wananchi wakicheza wakati Kikundi cha Shinyanga Arts kikitoa burudani kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.

Viongozi wa CCM na vijana wa hamasa UVCCM wakicheza wakati Kikundi cha Shinyanga Arts kikitoa burudani kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Moja ya bango wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakiteta jambo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Burudani ikiendelea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Burudani ikiendelea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakicheza na vijana kutoka NACOPHA wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwasili katika uwanja wa Sabasaba kwa ajili ya uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akitembelea mabanda wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” katika Mkoa wa Shinyanga.
Mabanda ya mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria
Wadau kutoka mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria na wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Wadau kutoka mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria na wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Wadau kutoka mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria na wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Wadau kutoka mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria na wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Mabanda ya mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria
Mabanda ya mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria
Mabanda ya mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria
Wananchi wakiendelea kupata huduma kwenye Mabanda ya mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria
Wadau kutoka mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria na wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Wadau kutoka mashirika/taasisi zinazotoa msaada wa kisheria na wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Picha mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria inayojulikana “Mama Samia Legal Aid Campaign” leo Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
0 comments:
Post a Comment