Monday, 12 June 2023

BARRICK YADHAMINI KONGAMANO LA WASOMI WA VYUO VIKUU LILILOANDALIWA NA TAASISI YA AIESEC KATIKA CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU AGUSTINI JIJINI MWANZA

...
Afisa Rasilimali watu mwandamizi wa Barrick Crispin Ngwaji, akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya mkoani Mwanza wakati wa kongamano la kuwajengea uwezo lililoandaliwa na taasisi ya kimataifa ya vijana isiyo ya kiserikali inayohamasisha masuala ya uongozi na kujitolea kwa Jamii ya AIESEC Tanzania na kudhaminiwa na Kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick, lililofanyika jijini Mwanza katika chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino mwishoni mwa wiki.
 *****

KAMPUNI ya Barrick nchini Tanzania, imedhamini na kushiriki katika kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu lililoandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AIESEC Tanzania) lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino jijini Mwanza na kuwashirikisha wanafunzi,wahadhiri na wadau mbalimbali.

Taasisi ya AIESEC inasifika kwa mchango wake mkubwa wa kuwajengea uwezo vijana ili kuwa viongozi bora na mahiri duniani kwa miaka ijayo. Nchini Tanzania pia taasisi hiyo inafanya kazi kwa kuwakutanisha vijana wenye ndoto ya kuwa viongozi bora hapo baadae ambapo pia inatoa fursa kwa vijana kujiunga.


Kupitia kongamano hili ambalo hufanyika kila mwaka, wanafunzi huweza kufahamu jinsi taasisi mbalimbali nchini zinavyoendesha shughuli zake lengo kubwa ikiwa ni kuwajengea uwezo wa kujua vipaji walivyonavyo, kujifunza jinsi ya kujiamini na kukabiliana na ushindani katika soko la ajira, kujitambua uwezo wao ni jinsi gani wanaweza kushiriki kutoa mchango wa kuendeleza taifa pindi wamalizapo masomo yao.


Wataalamu mbalimbali walitoa mada za kuwajengea uwezo Wanafunzi kusoma kwa bidii na kuzidi kuwa wabunifu ili waweze kwenda sambamba na mabadiliko ya kiteknolojia na kidigitali ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali za ajira zinazojitokeza na pia kuwa na uwezo wa kujiajiri.


Maofisa Rasilimali Watu Waandamizi wa Barrick pia walishiriki katika maonesho na kongamano hilo ambapo walipata fursa kuzungumza na wanafunzi kuhusiana na kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ajira,kuendeleza vipaji vyao pia wanafunzi walipata fursa kuelewa jinsi kampuni ya kimataifa ya Barrick, inavyoendesha shuguli zake kwa kutoa kipaumbele kusaidia jamii sambamba na mpango wake wa kuibua na ukuzaji wa vipaji kwa vijana wa kitanzania na wafanyakazi wake na mpango wa kampuni wa kufanikisha kutekeleza malengo endelevu ya milenia.


Afisa Mazingira wa jiji la Mwanza Fanuel Kasenene akiongea katika kongamano hilo alitoa wito kwa wanafunzi kutumia fursa za mafunzo kama haya ya kuwajengea uwezo kuhakikisha maarifa wanayipatiwa wanayatekeleza kwa vitendo badala ya kutegemea elimu ya taaluma zao tu na aliipongeza kampuni ya Barrick kwa jitihada inazofanya kuibua na kukuza vipaji vya vijana wenye viwango mbalimbali vya elimu na kuwapatia ajira sambamba na kuwawezesha kujiajiri.
Afisa Rasilimali watu wa Barrick North Mara, Daniel Paul, akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya mkoani Mwanza wakati wa kongamano la kuwajengea uwezo lililoandaliwa na taasisi ya kimataifa ya vijana isiyo ya kiserikali inayohamasisha masuala ya uongozi na kujitolea kwa Jamii ya AIESEC Tanzania na kudhaminiwa na Kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick, lililofanyika jijini Mwanza katika chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino mwishoni mwa wiki.
Afisa Mazingira wa jiji la Mwanza, Fanuel Kasenene, akiongea katika kongamano hilo

Wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya mkoani Mwanza wakifurahia jambo, wakati wa kongamano hilo.
Wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya mkoani Mwanza wakifurahia jambo, wakati wa kongamano hilo.
Wanafunzi wa vyuo vikuu vya mkoani Mwanza wakiskani codes ili kuingia kwenye fursa zilizopo katika kampuni ya Barrick nchini, wakati wa kongamano hilo.
Wanafunzi wa vyuo vikuu vya mkoani Mwanza wakiskani codes ili kuingia kwenye fursa zilizopo katika kampuni ya Barrick nchini, wakati wa kongamano hilo.
Picha ya pamoja ya baadhi ya wafanyakazi wa Barrick na viongozi wa AISEC wakati wa kongamano hilo
Picha ya pamoja ya baadhi ya wanafunzi na wadau mbalimbali walioshiriki katika kongamano hilo
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger