Thursday 15 June 2023

TGNP YAKUTANISHA WADAU KATIKA KIJIWE CHA KAHAWA KUFUATILIA MUBASHARA HOTUBA YA HALI YA UCHUMI NA BAJETI YA TAIFA IKISOMWA BUNGENI

...

Mkuu wa Program kutoka TGNP Bi. Clara Kalanga akifungua Mjadala na Uchambuzi wa Bajeti ya Taifa ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 maarufu Jukwaa la ‘Kijiwe cha Kahawa’ kwa niaba ya Mkurugenzi wa TGNP, leo Alhamis Juni 15,2023 katika ukumbi wa TGNP jijini Dar es salaam 

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) limekutanisha wadau wa masuala ya jinsia katika Mjadala na Uchambuzi wa Bajeti ya Taifa ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 maarufu ‘Kijiwe cha Kahawa’ ili kuwapa fursa kufuatilia mubashara Hotuba ya Hali ya Uchumi wa taifa 2022/2023 na Mpango wa Maendeleo ya taifa kwa mwaka 2023/2024 pamoja na Hotuba ya Bajeti ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 ikiwasilishwa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Akifungua Mjadala na Uchambuzi wa Bajeti ya Taifa ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 maarufu Jukwaa la ‘Kijiwe cha Kahawa’  kwa niaba ya Mkurugenzi wa TGNP, Mkuu wa Program kutoka TGNP Bi. Clara Kalanga leo Alhamis Juni 15,2023 katika ukumbi wa TGNP jijini Dar es salaam amesema lengo la Jukwaa la Kijiwe cha Kahawa ambalo limekuwa likiandaliwa na TGNP kwa miaka minne sasa ni kuwapa fursa wadau mbalimbali kufuatilia hutoba ya bajeti Mubashara na kuweza kutoka maoni na mapendekezo yao yatakayowezesha uboreshaji wa utekelezaji wake kwa mrengo wa kijinsia.

“Kwa mwaka huu dhima ya Kijiwe cha Kahawa ni kuhamasisha dhana ya ushirikishwaji kwa makundi yote ili kuandaa na kutekeleza bajeti zenye mrengo wa kijinsia ‘Promoting inclusive budgetary process for a gender responsive 2023/2024 budget”,amesema Kalanga.

Ameeeza kuwa Kijiwe cha Kahawa ni mojawapo ya majukwaa ya TGNP kujenga nguvu za pamoja ili kuleta chachu ya mabadiliko chanya ya kisera, kiutendaji na kifikra.

“Kukutana kwetu hapa ni kwa ajili ya kuhamasisha nguvu za pamoja katika kudai utengwaji wa bajeti kwa mrengo wa kijinsia ili kutatua changamoto za makundi mbalimbali katika jamii hasa yale yaliyo pembezoni kama vile wanawake, wanaume maskini, watu wenye ulemavu na vijana”,ameongeza Kalanga.

Amesema kwa miaka 30 sasa TGNP imekuwa mstari wa mbele katika kujenga uwezo na ushawishi juu ya bajeti yenye mrengo wa kijinsia na imekukuwa ikijihusisha na mchakato wa bajeti kila mwaka kwa kuwawezesha wanawake na makundi yaliyo pembezoni katika ngazi za jamii kushiriki kikamilifu kupitia mchakato wa fursa na vikwazo (O&OD) unaofanyika katika ngazi ya jamii kuweza kuibua vipaumbele vyao na pia kuwaunganisha na mjadala wa kitaifa ili kudai utengwaji wa rasilimali kwa ajili ya masuala ya jamii kwa ujumla.

“Tunaipongeza serikali kwa kutuonesha nia ya kuendeleza usawa wa kijinsia nchini kwa kuchukua hatua katika kutekeleza baadhi ya mapendekezo ambayo tumekuwa tukiyatoa kupiti chambuzi zetu za bajeti na kupitia ushiriki wa wadau mbalimbali. Hata hivyo tunaiomba serikali kutumia matokeo haya katika mipango na bajeti ili vipaumbele viendane na mahitaji ya makundi husika”,amesema Kalanga.

“Tunatambua na tunaendelea kupongeza jitihada za serikali yetu katika kuridhia utekelezaji wa mikataba mbalimbali ya kitaifa,kikanda na kitaifa ili kuendeleza usawa wa kijinsia nchini. Ili kuweza kutekeleza kwa ufanisi mikataba hii na sera na mipango mingineyo, Bajeti yenye mrengo wa kijinsia ni suala la msingi”ameongeza.

Amefafanua kuwa ikiwa rasilimali za kutosha hazitatengwa, hazitatolewa na kutekelezwa kwa wakati, kufikia usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu itakuwa ni ndoto.

Wakichangia hoja wakati wa majadiliano hayo, wadau hao wameipongeza serikali kwa kuanzisha huduma za kibingwa za matibabu katika Hospitali huku wakionesha wasiwasi juu ya huduma hizo za kibingwa kuwanufaisha wananchi waliopo maeneo ya pembezoni ambako hata zahanati tu hazipo na zingine zikiwa zinakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Mkuu wa Program kutoka TGNP Bi. Clara Kalanga akifungua Mjadala na Uchambuzi wa Bajeti ya Taifa ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 maarufu Jukwaa la ‘Kijiwe cha Kahawa’ kwa niaba ya Mkurugenzi wa TGNP, leo Alhamis Juni 15,2023 katika ukumbi wa TGNP jijini Dar es salaam. Picha na Kadama Malunde 1 blog
Mkuu wa Program kutoka TGNP Bi. Clara Kalanga akifungua Mjadala na Uchambuzi wa Bajeti ya Taifa ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 maarufu Jukwaa la ‘Kijiwe cha Kahawa’

Wadau wa masuala ya Kijinsia wakiwa katika Ukumbi wa TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam wakisikiliza mubashara Hotuba ya Hali ya Uchumi wa taifa 2022/2023 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2023/2024 ikiwasilishwa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger