Saturday, 17 June 2023

TBS YAKABIDHI VYETI NA LESENI 264 KWA WAZALISHAJI WA BIDHAA AMBAZO ZIMEKIDHI MATAKWA YA VIWANGO

...
Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt.Athuman Ngenya akikabidhi vyeti na leseni kwa wazalishaji wa bidhaa ambazo zimekidhi matakwa ya Viwango. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 17,2023 Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam

******************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limekabidhi vyeti na leseni 264 vikiwemo vyeti na leseni 257 za kuthibitisha ubora wa bidhaa pamoja na vyeti saba (7) vya kuthibitisha ubora wa mifumo (Management system certification).

vyeti na leseni zimetolewa kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia mwezi Oktoba, 2022 hadi Mei, 2023.

Akizungumza na Waandishi wa habari katika hafla hiyo ambayo imefanyika leo Juni 17,2023 Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt.Athuman Ngenya amesema leseni na vyeti 107 ambayo ni sawa na asilimia 41.6 vilitolewa kwa wajasiriamali wadogo wadogo.

Vyeti na leseni zilizotolewa ni za bidhaa za vyakula, vipodozi, vifaa vya ujenzi, vilainishi, vifaa vya umeme, trela, vibebeo, vifungashio pamoja na mifumo ya utoaji huduma.

Aidha amesema kwa kipindi cha kuanzia mwezi Oktoba 2022 mpaka Mei, 2023 wamekwisha sajili maeneo (maduka, maghala, magari) 1,394 ya kuuza, kuhifadhi au kusambaza bidhaa za vyakula na vipodozi. Pia, kwa kipindi hicho wameweza kusajili bidhaa 1255 za vyakula na vipodozi toka nje ya nchi.

Pamoja na hayo amewasisitizia wajasiriamali hao kuwa mabalozi wazuri katika matumizi ya Viwango ili kufikia lengo la Tanzania ya viwanda hasa katika kipindi hiki ambapo Tanzania tupo uchumi wa kati.

Hafla hiyo imebeba kauli mbiu ya ubora ya mwaka huu wa 2022/2023 inayosema “Dhamira bora fanya kwa usahihi”. Kauli mbiu hiyo ni ujumbe tosha kwa wazalishaji kuwa ubora wa bidhaa unaanza na nia njema ya kuzalisha bidhaa kwa kuzingatia matakwa ya sheria, kanuni na miongozo iliyopo kwa hiari na kwa usahihi, ili kuhakikisha watumiaji wanapata bidhaa bora muda wote.


Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt.Athuman Ngenya akikabidhi vyeti na leseni kwa wazalishaji wa bidhaa ambazo zimekidhi matakwa ya Viwango. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 17,2023 Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt.Athuman Ngenya akizungumza katika hafla ya utoaji vyeti na leseni kwa wazalishaji wa bidhaa ambazo zimekidhi matakwa ya Viwango. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 17,2023 Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora TBS, Bw.Lazaro Msasalaga akizungumza katika hafla ya utoaji vyeti na leseni kwa wazalishaji wa bidhaa ambazo zimekidhi matakwa ya Viwango. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 17,2023 Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam

Meneja wa Uthibitishaji bidhaa TBS, Bi.Amina Yasini akizungumza katika hafla ya utoaji vyeti na leseni kwa wazalishaji wa bidhaa ambazo zimekidhi matakwa ya Viwango. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 17,2023 Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger