Tuesday 13 June 2023

WANANCHI WAFURAHIA HUDUMA BORA ZA MATIBABU KITUO CHA AFYA BUGARAMA

...


Wananchi wafurahia huduma bora za matibabu kituo cha Afya Bugarama.

Na Marco Maduhu, KAHAMA

WANANCHI wa Bugarama Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga, wamepongeza huduma bora za matibabu ambazo zinatolewa katika Kituo cha Afya Bugarama na kuimarisha Afya zao, huku akina Mama Wajawazito wakijifungua salama.
Kitu cha Afya Bugarama

Wamebainisha hayo jana wakati wakiongea na Waandishi wa Habari kutoka Mkoani Shinyanga, ambapo wapo katika ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ambayo imetekelezwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kupitia fedha za (CSR) ikiwamo Sekta ya Afya.
Miundombinu ya Majengo ambayo yamejengwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu katika kituo cha Afya Bugarama.

Mmoja wa Wananchi hao Robert Nkwambi ambaye pia ni Mchimbaji mdogo wa Madini ya dhahabu, amesema kutokana na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kuboresha miundombinu katika Kituo hicho cha Afya na kuwezesha Vifaa Tiba, wamekuwa wakipata huduma bora za matibabu na kuimarisha Afya zao.
Mwananchi Robert Nkwabi akipongeza huduma bora za matibabu katika kituo cha Afya Bugarama.

“Awali Kituo hiki cha Afya ilikuwa ni Zahanati hapakuwa na huduma bora za matibabu, ambapo ilikuwa tulizamika kwenda hadi wilayani Kahama umbali mrefu, lakini baada ya Mgodi kuiboresha sasa hivi huduma zote za matibabu tunazipata hapa,”amesema Nkwabi.
Miundombinu ya Majengo ambayo yamejengwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu katika kituo cha Afya Bugarama.

Naye Mwanamke Zawadi Simba, anasema wanaushukuru Mgodi kwa kuboresha huduma za matibabu katika Kituo hicho cha Afya Bugarama zikiwamo na huduma za upasuaji kwamba wamekuwa wakijifungua salama.
Wananchi wakiendelea kupata huduma za matibabu katika kituo cha Afya Bugarama.

Naye Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Bugarama Dk. Silas Kayanda, amesema awali Wananchi wa Bugarama na vijiji jirani walikuwa wakipata shida kupata huduma bora za matibabu karibu, na hivyo kulazimika kufuata huduma hizo umbali mrefu wilayani Kahama Kilomita 73.
Mganga Mfawidhi kituo cha Afya Bugarama Dk. Silas Kayanda.

Amesema kutoka na kituo hicho cha Afya kuboreshwa na kuwezeshwa Vifaa Tiba vya kisasa wamekuwa wakipokea wagonjwa wengi tofauti na hapo awali, na wamekuwa wakidhalisha Wajawazito 180 hadi 250 kwa Mwezi, na Aprili mwaka huu walipokea pia Gari la Wagonjwa (Ambulance) kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Wananchi wakipata huduma za matibabu kituo cha Afya Bugarama.

Aidha, amesema Mgodi huo wa Barrick Bulyanhulu katika kuendelea kukiboresha kituo hicho cha Afya, pia wametoa kiasi cha fedha Sh.milioni 120 kwa ajili ya ujenzi wa uzio.
Miundombinu ya Majengo ambayo yamejengwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu katika kituo cha Afya Bugarama.

Naye Kaimu Meneja Mahusiano ya Jamii kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Zuwena Senkondo, amesema Mgodi huo umekuwa ukiwathamini Wananchi wanaouzunguka na kuwapatia huduma mbalimbali kupitia fedha za (CSR) na kuwatekelezea miradi ya maendeleo ikiwamo ya Sekta ya Afya.
Kaimu Meneja Mahusiano ya Jamii kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Zuwena Senkondo.

Amesema katika kituo hicho cha Afya Bugarama, wamejenga tena Jengo la Mionzi ili kiendelee kutoa huduma bora za matibabu kwa wananchi, na kubainisha pia katika Kata ya Ntobo wamejenga Chuo cha Uuguzi ambacho kitakuwa kikitoa wataalamu na kuondoa tatizo la upungufu wa watumishi katika Sekta ya Afya.
Muonekano wa Majengo ya ujenzi wa Chuo cha Uuguzi Kata ya Ntobo Halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger