Wednesday, 14 June 2023

SERIKALI YASISITIZA KUFANYA KAZI KWA KARIBU NA VYAMA VYA WAFANYAKAZI

...



Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Mhe. Ummy Nderiananga, akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti maalum (Chadema), Mhe. Sophia Mwakagenda kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu leo Juni 14,2023 bungeni jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, DODOMA

SERIKALI imesema itaendelea kufanya kazi kwa karibu na vyama vya wafanyakazi kwa kusuluhisha migogoro iliyopo kwenye baadhi ya vyama.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Mhe. Ummy Nderiananga ametoa kauli hiyo bungeni Juni 14, 2023 alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti maalum (Chadema), Mhe. Sophia Mwakagenda kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Katika swali lake, Mbunge huyo amehoji serikali inatoa kauli gani kuhusu ulazima wa kujiunga na vyama na itoe tamko la kuruhusu mwalimu kujiunga kujiunga na chochote anachoridhika nacho.

Akijibu swali hilo, Ummy amesema zipo katiba zinazoongoza vyama vya wafanyakazi na serikali inafahamu kuna baadhi ya vyama vina migogoro na serikali itaendelea kufanya kazi kwa karibu na vyama hivyo kwa kuboresha mapungufu yaliyopo na kusuluhisha migogoro.

“Niwatoe hofu walimu waendelee kukiamini chama chao cha walimu na sisi serikali tupo pamoja nao,”amesema.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger