Tuesday, 20 June 2023

MBUNGE MTATURU APAZA SAUTI YA WAFUGAJI BUNGENI

...


MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu,wakati akiuliza swali la nyongeza bungeni jijini Dodoma katika swali la msingi alilouliza kwa niaba ya Mbunge wa Kondoa Mjini Ally Makoa aliyetaka kujua ni lini serikali itajenga majosho katika Kata za Kolo,Kingale na Bolisa.

Na Mwandishi Wetu-DODOMA

MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameipongeza serikali kwa kuendelea kuboresha afya ya mifugo kupitia majosho wanayojenga nchini.

Pamoja na pongezo hizo ameihoji serikali ni lini itajenga josho katika Kata ya Siuyu iliyopo Wilayani Ikungi Mkoani Singida ili kuweza kutoa huduma ya mifugo katika Kata hiyo.

Mtaturu ameuliza swali hilo Bungeni Jijini Dodoma Juni 20,2023,wakati akiuliza swali la nyongeza katika swali la msingi alilouliza kwa niaba ya Mbunge wa Kondoa Mjini Ally Makoa aliyetaka kujua ni lini serikali itajenga majosho katika Kata za Kolo,Kingale na Bolisa.

“Kwa sababu majosho haya yanalenga katika kuboresha afya ya mifugo na mwisho wa siku tunapata kitoweo kizuri,nini mkakati wa serikali wa kuhakikisha kwamba ujenzi ule unasimamiwa vizuri na majosho yanakamilika kwa muda uliopangwa,

“Kwenye Jimbo la Singida Mashariki katika Kata ya Siuyu tulikuwa na josho ambalo sasa hivi limeingiliwa na eneo la kanisa la RC, na tuliomba lihamishwe liende eneo lingine kwa sababu linakosa sifa ya kutumika pale,tumeshatenga eneo katika kijiji cha Siuyu na tuliomba muda mrefu zaidi ya miaka mitatu,Je ni lini serikali itajega josho kwa ajili ya kutoa huduma ya mifugo katika kata ya Siuyu,”?amehoji.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi David Silinde amemuondoa hofu mbunge na kusema Wizara hiyo chini ya Waziri wake Abdallah Ulega na walio chini yake wameahidi kutekeleza yote waliyoyapanga katika mwaka wa fedha wa 2023/2024.

“Yale ambayo hayajakiamilika tutahakikisha katika mwaka wa fedha unaokuja yanakamilika kwa wakati,kwa sababu hili ndio lengo letu na ndio lengo la Mh Rais Samia Suluhu Hassan,

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa josho katika Kata ya Siuyu,Silinde amesema amelipokea na kuliwekea kipaumbele.

“Mh Mbunge amezungumzia josho katika Kata ya Siuyu,nimwambie tu nimelipokea,nitaangalia katika orodha niliyonayo kama tumeliweka ,na kama halipo tutaona namna gani tunatafuta fedha ili tuliweke katika moja ya kipaumbele chetu,”amesema.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger