Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota ameweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga iliyopo mtaa wa Shunu kata ya Nyahanga Manispaa ya Kahama.
Askofu Bugota ameweka jiwe la Msingi la Mradi wa ujenzi wa nyumba ya Kiaskofu leo Jumamosi Juni 17,2023 ambayo ni moja ya kazi za kitume zikiwa ni utekelezaji wa mpango mkakati wa Kanisa la AICT ambao unajishughulisha na malengo matano ya Kimkakati (Waefeso 2:10).
Akizungumza wakati akiweka jiwe hilo la msingi, Askofu Bugota amewapongeza na kuwashukuru waumini wa Kanisa la AICT ‘The Champions’ walioanzisha hoja ya kujenga nyumba ya Kiaskofu huku akisisitiza kuwa nyumba hiyo itafunguliwa mwezi Agosti,2023 wakati wa wiki ya maombi.
“Hii ni hatua nzuri na kubwa sana baada ya kupewa Dayosisi teule ya Shinyanga na Simiyu. Wakati tunafanya wiki ya maombi mwezi Agosti, Askofu Mkuu atafungua nyumba hii ili tulale humu”,amesema Askofu Bugota.
“Tunamshukuru sana Mungu kila mahali kanisa la AICT tumekuwa na watu ambao tunawaita The Champions wanaanzisha maono hata kama wengine tunafuata baadae kwa kusuasua lakini nashukuru sana kwa taarifa hii sasa kwamba huduma hii iliyoanzishwa na The Champions leo hii imekuwa huduma inayoungwa mkono na waumini wote”,amesema Askofu Bugota.
Ameeleza kuwa Baraza la Utendaji la AICT katika vikao vyake vya kawaida lilitoa ushauri katika Sinodi kuu iliyopita kwamba kanisa liendelee kupanua huduma ya injili nchini kwa hiyo Dayosisi ya Shinyanga imepewa jukumu la kuanzisha Dayosisi mbili mpya ambazo ni Kahama na Simiyu na tayari wameshaunda kikosi kazi cha kushughulikia uanzishwaji wa hizo Dayosisi.
“Kwa hiyo tunapoweka jiwe la msingi katika nyumba hii tunataka kutambulisha tu kwamba msingi wetu sisi kama waumini ni Yesu Kristo, huo ndiyo msingi imara, na kama Yesu atakuwa sehemu ya msingi katika Maisha yetu, tunaamini hata changamoto nyingi za kijamii tunazopambana nazo leo zitakuwa hazipo, maana Yesu hutengeneza upendo, Maisha ya uadilifu na anatupa pia matumaini ya milele na hata kama tunapita katika changamoto za Maisha Yesu ndiyo anabaki wa kutegemewa”,ameongeza Askofu Bugota.
“Tutumie nafasi hii kumsimamisha Yesu katika Maisha ya watu. Nyinyi wenyewe mnashuhudia wakati ambapo tunazungumzia ukatili wa Maisha, mmomonyoko wa maadili katika taifa hili. Serikali na sisi viongozi wa dini umekuwa wimbo wa mchana na usiku kukemea maovu hayo.
Tunaona tamaduni zinabadilika na tunaingia kwenye makosa ambayo kwa kweli hata ubinadamu haupo, leo hii wanaume kwa wanaume wanaweza kuoana au wanawake kwa wanawake wanaweza kufunga ndoa, katika mamlaka ya Mungu ni kinyume cha neno la Mungu. Sisi waumini na watumishi wa Mungu tutasimama katika neno hilo hadi siku ya kufa kuwaambia watu kuwa huo ni uovu na siyo msingi wa neno la Mungu”,amesema Askofu Bugota.
Akisoma taarifa fupi ya ujenzi wa nyumba ya utumishi (Kiaskofu), Katibu wa Kanisa la AICT Jimbo la Kahama Mjini, John Mtumai amesema mpaka sasa nyumba hiyo ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 80% inakadiriwa kutumia rasilimali vitu vya ujenzi na rasilimali fedha kiasi cha shilingi Milioni 100.
Amefafanua kuwa kutokana na mwamko mkubwa wa kanisa wenye kiu ya maendeleo ya kanisa, Ono la kujenga nyumba hiyo ilianza na wadau wa maendeleo ambao ni wazalendo wa kanisa wachache walionunua kiwanja na kukikabidhi kwa kanisa kisha ujenzi ulianza kwa kasi.
“Nitumie fursa hii kuwatambua wabeba maono wa kazi hii kubwa kwa kanisa na kuleta hamasa kwa kanisa letu la AICT ni Mwinjilisti Mathias Mtolo, Amos Sospeter, Charles Daudi Machali na Elisha Amos. Watumishi hawa wa Mungu wamefanya kazi kubwa sana kiu yao ni kuona kanisa letu linapata maendeleo na huduma ya Krsito na hivyo kuwepo kwa hamasa katika makanisa yetu ndani na nje ya Jimbo la Kahama na sasa kazi hii inaungwa mkono na kanisa lote la AICT”,ameeleza Mtumai.
“Pamoja na kazi hii ya ujenzi wa nyumba hii ambayo ni makazi ya Askofu mtarajiwa wa Dayosisi tarajiwa ya Kahama ambaye atakaa humo, mipango mingine ya muhimu kuanza nayo ni ujenzi wa nyumba moja ya katibu wa Dayosisi teule ya Kahama ambapo tayari kiwanja kipo”,amesema Mtumai.
Mtumai ameitaja mipango mingine ni kununua magari matatu ya ofisi ya Dayosisi teule (mpango upo), kuanzisha vitega uchumi vya dayosisi mfano shule, hospitali, vituo vya kati ambayo vitaleta maendeleo katika kanisa sambamba na eneo la kujenga ofisi za dayosisi na Kanisa la Uaskofu (Cathedtral) ambapo kiwanja kipo mtaa wa Malunga – Kahama chenye ukubwa wa hekari tatu na kina ramani ya mipango miji.
Sambamba na uwekaji jiwe la msingi la nyumba ya Kiaskofu pia kumefanyika harambee kwa ajili Ujenzi wa nyumba ya Kiaskofu katika Kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga itakayofunguliwa mwezi Julai 2023 kwa ajili ya kuweka vigae na kumalizia ujenzi wa nyumba ya kiaskofu Dayosisi teule ya Kahama ambayo itafunguliwa mwezi Agosti 2023.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota akizungumza wakati akiweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga leo Jumamosi Juni 17,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota akiongoza ibada wakati akiweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga leo Jumamosi Juni 17,2023.
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota (wa tatu kushoto) akikata utepe wakati akiweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga leo Jumamosi Juni 17,2023.
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota (wa tatu kushoto) akikata utepe wakati akiweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga leo Jumamosi Juni 17,2023.
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota (wa tatu kushoto) akikata utepe wakati akiweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga leo Jumamosi Juni 17,2023.
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota akiweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga leo Jumamosi Juni 17,2023.
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota akiweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga leo Jumamosi Juni 17,2023.
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota akisoma maandishi baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga leo Jumamosi Juni 17,2023.
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota akiomba baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga leo Jumamosi Juni 17,2023.
Muonekano wa nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga
Muonekano wa nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga
Viongozi na waumini wa Kanisa la AICT wakiongozwa na Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota wakiwasili katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga
Viongozi na waumini wa Kanisa la AICT wakiwa katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga
Katibu wa Kanisa la AICT Jimbo la Kahama Mjini, John Mtumai akisoma taarifa fupi ya ujenzi wa nyumba ya utumishi (Kiaskofu) Dayosisi teule ya Kahama
Katibu wa Kanisa la AICT Jimbo la Kahama Mjini, John Mtumai akisoma taarifa fupi ya ujenzi wa nyumba ya utumishi (Kiaskofu) Dayosisi teule ya Kahama
Katibu wa Maendeleo , Mipango na Uchumi Kanisa la AICT Jimbo la Kahama Mjini, Mwinjilisti Mathias Mtolo akizungumza wakati Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota akiweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama. Wengine ni wabeba maono wa kazi hiyo ya ujenzi wa nyumba ya kiaskofu
Mhasibu Msaidizi wa kamati ya uchumi, mipango na maendeleo ya Kanisa la AICT Kahama Mjini, Charles Daudi Machali akizungumza wakati Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota akiweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama.
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota akiongoza maombi baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota akiongoza maombi baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama
Muonekano wa Kanisa la AICT Kahama Mjini
Muonekano wa Kanisa la AICT Kahama Mjini
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
0 comments:
Post a Comment