*************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Klabu ya Yanga imeichapa mvua ya magoli timu ya Dodoma Jiji mabao 4-0 katika mchezo wa NBC Premier league uliochezwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Yanga imecheza kandanda safi ambapo mshambuliaji wao mahiri Fiston Mayele...
Friday, 31 December 2021
NAMUNGO YATAMBULISHA MAKOCHA WAPYA

Klabu ya Namungo imetangaza benchi jipya la ufundi la klabu hiyo. Imemtambulisha Hanour Janza ambaye ni raia wa Zambia kuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo akisaidiwa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambaye atakuwa kocha msaidizi....
RAIS SAMIA ATEUA VIONGOZI MBALIMBALI... YUMO JAKAYA KIKWETE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.
Miongoni wa walioteuliwa ni Rais mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Jakaya Kikwete kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Chancellor) kwa kipindi kingine...
MREMBO AIBA MTOTO ILI KUNUSURU NDOA YAKE 'KAKOSA MTOTO MUDA MREFU'

JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia mkazi wa Buhongwa jijini humo, Rose Joshua (27) kwa tuhuma ya wizi wa mtoto wa kiume.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhan Ng’anzi amesema kuwa, tukio hilo lilitokea Desemba 19, mwaka huu, saa 4:00 usiku katika eneo la Dampo Soko la Machinga,...
MWANAMKE AJIFANYA KAHABA, AWALEWESHA WANAUME KISHA KUWAIBIA

JESHI la Polisi nchini Kenya wanamshikilia mwanamama Joyce Aluta wa Mombasa kwa kosa la kuwawekea wanaume dawa za kulevya kwenye pombe na kisha kuwaibia vitu mbalimbali kama simu, saa, viatu, wallet na pesa.
Joyce mwenyeji wa eneo la Kisimani, Nyali anadaiwa wakati mwingine kujifanya kahaba na...
MHUDUMU WA BAA AMUUA MWENZAKE KWA CHUPA WAKIGOMBANIA CHENJI 2500 ILIYOACHWA NA MTEJA
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia mhudumu wa baa Pendo Mwakifamba (21) kwa tuhuma za mauaji ya Hilda Mwambona (25) kwa kumkata na chupa sehemu mbalimbali eneo la tumboni.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Urlich Matei amesema tukio hilo limetokea jana wakati mtuhumiwa na marehemu wakigombea...
MKE AMUUA MUMEWE KWA KUMCHOMA MOTO SINGIDA

Mwalimu wa Sekondari ya New Kiomboi mkoani Singida, Simon Roman (33) amefariki dunia baada ya kuchomwa moto na mkewe sababu ikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Tukio hilo lilitokea Desemba 27, 2021 jioni baada ya mume kurudi kutoka matembezi huku mkewe akitaka kujua kuhusu uhusiano wa mumewe na...
WADAU WAJADILI MIKAKATI YA KAMPENI SHIRIKISHI YA KINGA DHIDI YA UVIKO 19…HALMASHAURI KUCHANJA WATU 500 KILA SIKU SHINYANGA
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza wakati akifungua kikao cha wadau kwa ajili ya kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkoa wa Shinyanga...
Thursday, 30 December 2021
NAIBU WAZIRI ATOA SIKU 14 KWA KIWANDA KUREKEBISHA MFUMO WA MAJI TAKA

Kiwanda cha Hengji Investment Ltd cha Jijiji Dar es Salaam hii leo Desemba 30, 2021 kimepewa siku 14 kuhakikisha kinaweka mfumo wa kutibu maji taka kabla ya kuyatiririsha kwenye mazingira kufuatia agizo lililotolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamad Chande...
MWANAMKE MWINGINE AUAWA JIJINI ARUSHA
Happy Lazaro, Arusha
Mwanamke mwingine mkazi wa Njiro, jijini Arusha,Janerose Dewasi(66) ameuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali na anayetuhumiwa ni mfanyakazi wake wa ndani.
Tukio hili limetokea siku chache baada ya mwanamke mwingine,Ruth Mmasi kubainika kuuawa eneo la Njiro...
AZAM FC YAMSAINISHA IBRAHIMU AJIBU

***********
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Klabu ya Azam Fc imefanikiwa kuinasa saini ya Ibrahimu Ajibu akitokea klabu ya Simba Sc mara baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa.
Ajibu amekuwa miongoni mwa wachezaji wakipekee waliochezea timu kubwa mbili ambazo ni mahasimu yaani...
NHC KUANDAA KAMPENI KABAMBE YA UKUSANYAJI MADENI KWA WADAIWA SUGU

Meneja wa Huduma na Uhusiano wa NHC, Bw.Muungano Saguye akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam. Meneja wa Huduma na Uhusiano wa NHC, Bw.Muungano Saguye akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ofisi za Shirika hilo leo Jijini Dar es...
Wananchi Muhimbili ‘wafunguka’ Mbele Ya Waziri Gwajima
Na Atley Kuni, WAMJW, DSM.
Wananchi na wazazi wanaopata huduma kwenye kliniki ya watoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamemuomba Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuongezewa wataalam wa huduma ya mishipa ya ubongo.
Wakizungumza mbele ya Waziri wa Afya Dkt. Dorothy...
Wednesday, 29 December 2021
TUME YA UTUMISHI WA WALIMU YATAJA MAKOSA VINARA KWA UTOVU WA NIDHAMU KWA WALIMU..YAMO MAPENZI
Mwenyekiti wa TSC Profesa Willy Komba akiongea na waandishi wa habari Jijini Dodoma (hawapo pichani) kuhusu mwenendo wa maadili ya utumishi wa walimu nchini
***
Na Dotto Kwilasa Malunde 1 blog, DODOMA.
TUME ya Utumishi wa Walimu Nchini (TSC) imetaja makosa ambayo ni vinara...
Tuesday, 28 December 2021
RAIS MWINYI ATEUA VIONGOZI WANNE
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
***
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameteua wafuatao kuwa makamishina wa Tume ya Kurekebisha Sheria.
Mosi kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza...
RAIS SAMIA : TUTAENDELEA KUKOPA ILI KUMALIZA MIRADI YA MAENDELEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
**
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kwamba serikali yake itaendelea kukopa kwa lengo la kumaliza na kuikamilisha miradi yote ya maendeleo.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 28, 2021, jijini Dar es Salaam,...
Tanzia : MWANAMUZIKI MAARUFU GENERAL DEFAO AFARIKI DUNIA
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema mwanamuziki mahiri wa Rhumba Le General Defao Matumona amefariki dunia akiwa nchini Cameroon Taarifa zaidi tutawaletea hivi punde
Defao alizaliwa Desemba 03, 1958 katika jiji la Kinshasa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Baada ya kuzaliwa...