MHITIMU wa Shahada ya Uzamivu kutoka Chuo cha Afya KCMC katika taaluma ya Huduma ya Afya ya Jamii, Maseke Mgalo ameeleza kuwa tafiti aliyofanya juu ya upatikanaji na utoaji wa huduma ya afya ya jamii, amebaini kuwa kundi la wavuvi linaendelea kupata maambukizi ya VVU kutokana na mazingira yao.
“Licha ya mtu wa kwanza Afrika kupata maambukizi ya VVU alitoka katika kundi la wavuvi bado kundi hilo halifikiwi kwa urahisi kupatiwa elimu ya afya kutokana na mazingira yao pamoja na tabia yao ya kununua ngono.
“Nilifanya utafiti wangu Mkoa wa Mwanza na Mara vijijini wavuvi bado wana hatari ya kupata mambukizi ya VVU kwani bado wanafanya biashara ya ngono hadi Tsh 3000, hii ni hatari nimependekeza serikali ipeleke elimu huko kunusuru kundi hilo muhimu kwa jamii,” Maseke Mgalo, Phd.
0 comments:
Post a Comment