Sunday 28 November 2021

Tanzia : NGULI WA PICHA TANZANIA RAMADHANI TONGE AFARIKI DUNIA

...



Mzee Ramadhani Tonge ambaye aliwahi kuwa mkufunzi wa masuala ya picha katika vyuo vya uandishi wa habari jijini Dar es Salaam amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Amana, Ilala  Jijini  Dar es Salaam na mwili wake utasafirishwa kwenda Morogoro kwa ajili ya mazishi.

Kwa nyakati tofauti, Mzee Tonge alitoa huduma ya ukufunzi katika Chuo cha Uandishi wa Habari cha Times School of Journalism (TSJ) cha Ilala Shariff Shamba jijini Dar es Salaam.

Pia aliwahi kuwa mkufunzi Dar es Salaam School of Journalism kilichopo Ilala, Sharrif Shamba na kuhudumu SHIHATA, Idara ya Habari MAELEZO na kwingineko kama mpiga picha.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger