Friday 26 November 2021

ASKARI MAGEREZA AJILIPUA NDANI YA NYUMBA YAKE

...


Wakaazi wa Lessos eneo bunge la Kwanza, Kaunti ya Trans Nzoia nchini Kenya waliamkia habari za kusikitisha kumhusu askari jela (magereza) aliyejilipua ndani ya nyumba yake Jumatano, Novemba 24 usiku. 

Elias Kipchumba Too ambaye alikuwa zamuni usiku alitoroka kutoka kituo chake cha kazi akiwa na bunduki aina ya G-3 ambayo alitumia kukatiza maisha yake.

Afisa wa gereza la kati la Kitale Julius Kaliakamur, alithibitisha kutokea kwa kisa hicho na kusema kuwa askari huyo mwenye umri wa miaka 25 hakuacha kijibarua chochote cha kueleza sababu za kujitoa uhai. 

Kwa mujibu wa ripoti ya K24, afisa huyo hakuonesh dalili zozote za kutatizika kimawazo.

 “Elias alikuwa zamu jana usiku. Kisha akatoka kisiri akiwa na bunduki yake, baadaye ikagundulika hakujulikana alipo na tukaingiwa na wasiwasi. Tulikimbia hadi nyumbani kwake eneo la Lessos na tukampata amefariki dunia," Kaliakamur alisema.

 Alifichua kuwa afisa huyo ambaye amekuwa akihudumu kwa miaka mitatu alikuwa ameomba uhamisho suala ambalo Huduma ya Magereza ya Kenya ilikuwa ikishughulikia.

"Uhamisho ni wa kawaida katika utumishi, tulipokea maombi yake ya uhamisho na kupeleka kwa mkuu wa gereza la mkoa ambaye alikuwa akiyashughulikia" aliongeza. 

Alimtaja afisa huyo kuwa mtu mkarimu ambaye alitekeleza majukumu yake mara moja na alisikitishwa mno na hatua yake kujitia kitanzi. 

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika makafani ya hospitali ya Cherangany Nursing Home ukisubiri kufanyiwa upasuaji.

 Kwingineko afisa wa GSU Jumanne, Novemba 23 aliuawa kwa kupigwa risasi na mwenzake katika hali isiyoeleweka huko kijiji cha Mitete eneo la Laikipia Magharibi.

 Akithibitisha kisa hicho, kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Laikipia John Nyoike alisema maafisa hao wawili walikorofishana katika kambi ya GSU eneo hilo kabla ya mmoja wao kutwaa bunduki yake na kumvamia mwenzake. 

Baada ya tukio hilo, afisa huyo aliyekuwa amejihami alikusanya mali yake ikiwemo bunduki aliyotumia katika kumshambulia mwenzake na kisha akaondoka.

 Juhudi za kumkamata afisa huyo ambaye aliingia mafichoni baada ya tukio hilo ziliambulia patupu kwani alikuwa akitoroka huku akiwafyatulia risasi wenzake waliokuwa wakimfukuza.

Kamanda wa polisi alisema uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha shambulio hilo huku msako dhidi yake ukianzishwa.

Chanzo - Tuko News
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger