Saturday, 27 November 2021

RAIS SAMIA ATEUA VIONGOZI MBALIMBALI, YUMO BALOZI OMBENI SEFUE

...





RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao:-

Mosi, amemteua Balozi Ombeni Yohana Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute). Balozi Sefue anachukua nafasi ya Dkt. Stergomena Tax ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 27, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Jafar Haniu, uteuzi huo umeanza tarehe 24 Novemba, 2021.


Pili amemteua Balozi Mathias Meinrad Chikawe, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mwenza wa Kampuni ya Uwakili ya FMD Legal Consultants and Advocates kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Tanzania and Italian Petroleum Refining Company Limited (TIPER).


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 27, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Jafar Haniu, uteuzi huo umeanza tarehe 24 Novemba, 2021.


Tatu amemteua Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe, Katibu Mkuu Mstaafu – TAMISEMI kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 27, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Jafar Haniu, uteuzi huo umeanza tarehe 16 Novemba, 2021.


Nne amemteua Prof. Ephata Elikana Kaaya kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Kilimanjaro (KCMUCo), Kilimanjaro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Saratani Ocean Road.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 27, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Jafar Haniu, uteuzi huo umeanza tarehe 15 Novemba, 2021.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger