Friday, 26 November 2021

DED NICE MUNISSY : WAZEE WA KIMILA WASHIRIKWISHE KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA

...

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy 
***
Na Mwandishi wetu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy amewataka wadau mbalimbali zikiwemo asasi za kiraia mkoa wa Shinyanga  kuwatumia wazee wa kimila katika mapambano ya kupinga ukatili kwa halmsahuri ya wilaya ya Shinyanga.

Munissy ametoa rai hiyo Novemba 24, 2021 wakati wa mafunzo yaliyotolewa kwa asasi za kiraia na shirika la Mfuko wa Wanawake Tanzania(WFT) kuhusu tathmini ya utekelezaji wa MTAKUWWA katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Alisitiza kuwa wazee wa kimila katika halmashauri ya Shinyanga wanaheshimika na wana kundi kubwa la watu hivyo ni jambo la muhimu kwa wadau kutambua ushiriki wao katika kutokomeza ukatili kwa mkoa wa Shinyanga.

Alieleza kuwa itakuwa ni kazi rahisi katika utekelezaji wa kutokomeza ukatili iwapo wazee wa kimila watapewa elimu ili watambue mila zipi ni nzuri na mbaya.

 "Tusikubali kuendelea kujielimisha wenyewe kila wakati,semina kama hizi ni muhimu na wazee wa kimla kushirikishwa kila mara kwa ajili ya kuleta mabadiliko", alisema Munissy.

"Historia ya miaka mitatu wa halmashauri ya Shinyanga kuhusu ukatili kwa wanawake na watoto imepungua tofauti na miaka ya nyuma. Changamoto ni uhaba wa watumishi ili kuweza kusaidia kutokomeza ukatili kwa halmashauri yetu",aliongeza.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngasa Mboje alizitaka asasi za kiraia kuweka juhudi za kuwatumia waganga wa kienyeji katika kupinga ukatili kwa kuwa ni kundi linalokusanya watu wengi kwa matibabu ikiwa ni wanawake na watoto.

"Jamii yetu inaamini, kutambua ma kuwapa heshima wazee wa kimila,tusipowapa nafasi kwa kuwapa elimu, juhudi zetu zitachelewa kuwakomboa watoto na wanawake. Halmashauri yetu ipo tayari kuweka bajeti juu ya maeneo yanayohitaji bajeti katika kupinga ukatili kwa halmashauri yake",alisema.

Mkurugezi wa shirika la ICS,Kudely Sokoine alisema masuala ya mila na desturi ni mzizi wa ukatili na jamii ya watu inaheshimu sana wazee wa kimila hivyo ni muhimu kubadili mitizamo na kupata matokeo kwa mikakati kwa kujikita zaidi kwa wazee wa kimila
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy akiwa ukumbini
Afisa kutoka WFT Neema Msangi akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngasa Mboje
Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC), Estomine Henry akielezea namna klabu hiyo inashiriki katika kutokomeza ukatili wa kijinsia kwenye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Aisha Omary akizungumza katika mafunzo hayo.
Mkurugezi wa shirika la ICS,Kudely Sokoine akifuatilia mafunzo ukumbini
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger