Monday, 11 March 2019

WAZIRI AAGIZA WANASIASA WAHUNI WANAOMTUKANA RAIS MAGUFULI WAKAMATWE

...

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ameagiza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa wanasiasa ambao wanafanya mikutano ya ndani ambayo imepigwa marufuku.

Kangi Lugola ametoa kauli hiyo akiwa Mkoani Morogoro wakati akizungumza na wananchi wa Mjini Kilosa ambapo amesema ana taarifa za kuwepo kwa baadhi ya wanasiasa wa upinzani wanaofanya vikao vyao vya ndani huku wakitoa kauli ambazo zinaashiria uchochezi.

“Mimi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, sitakubaliana na kiongozi wa chama chochote kuvunja agizo tulilolitoa nchi nzima kwa kutoruhusu kufanyika mikutano ya hadhara ya siasa, na pia kupitia mikutano ya ndani ambayo inafanyika, baadhi ya wanasiasa wahuni wanamtukana Rais ambaye ndiyo kiongozi Mkuu wa nchi, mimi sitakubaliana na hilo,” amesema Lugola.

Aidha Lugola amesema Rais Magufuli ni kiongozi ambaye kwa muda mfupi ameiletea mabadiliko makubwa nchi na pia ana mipango mikubwa ya maendeleo yanayokuja katika uongozi wake.
Chanzo - EATV
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger