Wednesday 27 March 2019

Rais Magufuli ampangia kituo cha kazi aliekuwa Bosi TAKUKURU......Ateua Mwenyekiti wa Bodi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Richard Faustine Sambaiga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Sambaiga umeanza March 23, 2019.

Dkt. Sambaiga ni Mhadhiri Mwandamizi, Idara ya Sosholojia ya Chuo Kikuu cha DSM na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Rukia Masasi ambaye amemaliza muda wake.

Pia Rais Magufuli kesho March 28, 2019 atamuapisha Balozi Mteule Valentino Mlowola kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba.

Balozi Mteule Mlowola ataapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 3:30 asubuhi.



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger