Saturday, 29 August 2020

NMB Yaweka Mikakati kukuza utalii Tanzania

...

Meneja wa matawi ya NMB Zanzibar – Abdalla Duchi (kushoto) akimkabidhi hotuba yake Waziri wa Fedha Zanzibar- Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa aliyekua mgeni rasmi katika kongamano la Wadau wa Utalii Zanzibar. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Kadi wa NMB – Philbert Casmir. Meneja wa matawi ya NMB Zanzibar – Abdalla Duchi akizungumza kwenye kongamano la wadau wa sekta ya Utalii Zanzibar (ZATO) lililowaleta pamoja zaidi ya wadau 250 katika Hoteli ya Verde.


************************************

Benki ya NMB imesema kuwa inathamini sana sekta ya utalii nchini na imeweka mikakati endelevu zaidi katika kuhakikisha shughuli za utalii zinakuwa zaidi.


Hayo yamesemwa na Meneja wa matawi ya Benki ya NMB Zanzibar – Abdalla Duchi, wakati wa mkutano wa wadau wa utalii Zanzibar(ZATO) uliofanyika visiwani humo kwa udhamini mkuu wa Benki ya NMB.

Alisema Benki hiyo imejipanga vyema kutoa suluhisho la huduma za kifedha, kwa kuwa na mifumo bora zaidi ikiwemo ya ubadilishaji fedha na Biashara ya kadi ambayo imewezesha wataliii kutohangaika wanapofanya manunuzi na malipo mbali mbali kwa kushirikiana na mahoteli na baadhi ya makampuni ya utalii, walihakikisha wana mashine za malipo (POS) na pia kuimarisha mfumo wa malipo ya mitandano (E-Commerce).

Naye Mkuu wa Idara ya Biashara za kadi wa Benki ya NMB – Philbert Casmir alisema wanaimarisha huduma hizo ili kuhakikisha watalii wanapata huduma kupitia matawi ya Benki hio hasa pale yanapotokezea majanga ikiwemo Covid – 19 ambayo ilisitisha huduma nyingi.

Philbert Alifafanua kuwa Benki hiyo inaelewa katika kipindi cha Covid -19 biashara ikiwemo ya utalii na sekta ya hoteli zilipata changamoto. Hivyo, NMB ipo karibu zaidi na wateja wao ili kuhimili changamoto hizo zilizojitokeza.

Ametoa rai kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, wajumbe wa ZATO, na Wananchi wa Zanzibar kwa ujumla, kutumia Benki ya NMB kwani ipo kwa ajili yao, na ina mifumo thabiti ya kutoa suluhisho la huduma za kibenki, na ndiyo maana imetambuliwa na taasisi za kimatafa kama EURO Money kuwa ndio benki bora zaidi hapa nchini kwa miaka minane mfulululizo.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger