Sunday 28 June 2020

WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA KUANZA KUFANYA MTIHANI WAO WA MWISHO KESHO

...

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Dkt Charles Msonde

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Dkt Charles Msonde, amesema jumla ya watahiniwa 85,546 ndiyo waliosajiliwa kufanya mitihani ya kidato cha sita na ualimu inayotarajiwa kuanza nchi nzima hapo kesho Jumatatu Juni 29, 2020.

Msonde amesema maandalizi yote yameshakamilika na kupitia mtihani huo watahiniwa hao ndiyo watakuwa wanapimwa uelewa wao katika masomo waliyokuwa wakisoma.

Aidha baraza pia limezitaka kamati za mikoa za kusimamia mitihani kuhakikisha wanasimamia mitihani hiyo na kusitokee udanganyifu wowote kwa watahiniwa.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger