Wednesday, 24 June 2020

SERIKALI IMEFANIKIWA KATIKA VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA KWA ASILIMIA 90

...
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akikata utepe leo kuashiria uzinduzi wa kliniki ya Methadone katika Hospitali ya Bombo jijini Tanga.Kliniki hiyo imejengwa kwa thamani ya Sh milioni 17.Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigela na kushoto kwake ni Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) James Kaji
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akikata utepe leo kuashiria uzinduzi wa kliniki ya Methadone katika Hospitali ya Bombo jijini Tanga.Kliniki hiyo imejengwa kwa thamani ya Sh milioni 17.Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigela na kushoto kwake ni Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) James Kaji
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizungumza mara baada ya uzinduzi huo kulia ni Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) James Kaji
 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) James Kaji akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi huo kushoto ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu

 Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasiyoambukiwa Wizara ya Afya Dkt James Kiologwe akizungumza wakati wa uzinduzi huo  kushoto ni Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) James Kaji
 KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari akizungumza wakati wa halfa hiyo
 MKURUGENZI Mkazi wa Amref Health Africa Dkt Florence Temu akizungumza wakati wa uzinduzi huo
 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) James Kaji kushoto akiteta jambo na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy kabla ya uzinduzi huo katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizindua mpango wa Matibabu ya Methadone kwa waathirika wa Dawa za Kulevya jijini Tanga jana,Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akionesha mpango huo na kushoto kwake anayepiga makofi  ni Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) James Kaji
 Sehemu ya wadau mbalimbali wakifuatilia uzinduzi huo
Meneja wa NHIF Mkoa wa Tanga Ally Mwakababu akiwa na wadau wengine wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi huo

SERIKALI imefanikiwa katika vita dhidi ya mapambano ya uingizaji,matumizi ya dawa za kulevya kwa asilimia 90 tangu Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu pamoja na Kamisha Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) James Kaji katika hafla fupi ua uzinduzi wa kituo cha huduma za Methadone katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tanga ya Bombo leo.

Waziri Ummy ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa kituo hicho ambacho ujenzi wake umegharimu fedha kiasi cha Sh milioni 17 ambazo kati ya fedha hizo Sh milioni 14 zimetolewa na serikali ya Marekani kupitia mradi wa PEPFAR kupitia Shirika lilsilokuwa la kiserikali la Amref Health Africa.


Alisema na Sh milioni 3 zimetokana na fedha za ndani za hospitali asema kuwa katika kipindi hicho serikali katika juhudi zake imefanikiwa kuwakamata wauzaji wakubwa wa dawa za kulevya ambapo pia wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza matumizi ya dawa hizo.

Kituo hicho tangu kianze kazi Juni 15 tayari kina wateja 37 wanaotumia dawa za methadone.

Amesema kuwa kwa mujibu wa takwimu za Wizara kuhusu hali ya dawa za kulevya na maambukizi ya VVU nchini ya mwaka 2014 zinaonesha kuwa Tanzania inakadiriwa kuwa na jumla ya waathirika wa dawa za kulevya kati ya 200,000-350,000.


Ambapo kati yao waathirika takribani 30,000 wanatumia dawa zakulevya kwa njia ya kujidunga huku kukiwa na makadirio ya asilimia 35 ya kiwango cha maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa wanaojidunga wakati katika hali ya kawaida kila watu 100 wasiotumi a dawa watu 5 wana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Amefafanua kuwa baada ya mapambano hayo,hali ya maambukizi kwa kundi la watu wanaotumia dawa zakulevya kwa njia ya kujidunga imepungua kutoka asilimia 35 hadi asilimia 10 na kwa upande wa mkoa wa Tanga una zaidi ya waathirika wa dawa za kulevya 5,190 wa dawa za kulevya aina ya Heroin.


Alisema kiwango ambacho kinakadiriwa kuwa ni sawa na watu 47 watu wazima kwa kila watu 100,000 na hivyo kuufanya mkoa wa Tanga kuwa pili Tanzania kwa waathirika wa dawa za kulevya.

Amesema kuwa katika kuhakikisha mapambano hayo yanaendelea baada ya kuzidua kituo hicho cha Kliniki ya muda ya Methadone na kufanya Tanzania kuwa na vituo vya aina hiyo nane ambapo hadi sasa takribani waathirika 8,071 wanapatiwa huduma za Methadone ambapo kati yao wanawake ni 480 na wanaume ni 7,591.


Waziri huyo alisema Serikali inajenga jengo jingine la kudumu katika hospitali hiyo ya bombo lenye ghorofa tatu ujenzi ambao unakadiriwa kuwa kugharimu Sh milioni 736,705,586 fedha ambazo zinatolewa naMfuko wa Dunia(Global Fund) kupitia Wizara ya Afya pamoja na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) ambapo unatarajiwa kukamilika kabla ya Disemba 30 mwaka huu.

Aidha,ametaka pia vituo hivyo vijengwe kwenye hospitali zote katika ngazi za halmashauri ili viweze kuwahudumia watu wengi zaidi bila gharama ambapo vituo vingine vipo katika Jiji la Dar es Salaam katika hospitali za rufaa za Mwananyamala,Muhimbili na Temeke,mkoani Mbeya katika Hospitali ya Rufaa ya Nyanda zaJuu Kusini,Sekou Toure mkoani Mwanza,Bagamoyo mkoani Pwani na Itega mkoani Dodoma.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya,James Kaji amesema kuwa Tanzania ilisifiwa kwa kuonesha mafanikio katika vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya kwa asilimia 90 katika mkutano wa Kimatatifa uliofanyika Geneva nchini Uswisi mwezi Machi mwaka huu.

Amebainisha mafanikio ni kutokana na Mamlaka hiyo kukamata wafanyabiashara wa dawa za kulevya,kutoa elimu kwa jamii na kupunguza madhara kwa waathirika wa dawa za kulevya(harm reduction).

Amesema kuwa katika taarifa za dawa za kulevya za mamlaka hiyo mwaka 2019,walifanikiwa kukamata bangi tani 21,kuteketeza mashamba ya bangi ekari 22,kukakamata mirungi tani 9 na kilo 20 za dawa za kulevya aina uya Heroin,Cocaine kilo 10 na kuwakata watuhumiwa wa dwa za kulevya wapatao 10,384.

Ametoa wito kwa Watanzania kutowanyanyapaa waathirika wa dawa za kulevya badala yake wapelekwe kweny vituo vya kliniki za methadone.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigela amesema mkoa wa Tanga upo katika mapambano makuu matatu ya uingizwaji wa dawa za kulevya,upitishwaji wa magendo na waamiaji haramu,hivyo serikali ya mkoa inaweka juhudi zaidi katika kudhibiti hayo.

Mashuhuda watatu wa dawa za kulevya ambao wapo katika kliniki hiyo ya muda a Methadone mkoani hapa wamebainisha baadhi ya mambo yanayowafanya vijana wengi kujiingiza katika matumizi ya dwa za kulevya kuwa ni tama ya pesa,kujiingiza katika starehe na ushawishi.

Yusufu Salim mkazi wa Ngamiani Kati amesema yeye alijiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya tangu akiwa anasoma kidato cha tatu baada ya kutumika kuwa mbebaji wa dawa hizo kwa miaka 11 kwa tamaa ya kupata fedha nyingi.

Mwajuma Juma mkazi wa Dar es salaam amesema kuwa yeye aliingizwa katika matumizi ya dawa za kulevya kwa kushawishiwa na mume wake wakati Ally Juma mkazi wa Tanga anasema kuwa yeye alijiingiza katika matumizi hayo baada ya kuwa na pesa nyingi nakuona starehe kubwa nai hiyo.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger