Saturday 27 June 2020

NTOBI AJITOSA UBUNGE SHINYANGA MJINI

...

Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga, pia Mwenyekiti wa Umoja wa Madiwani CHADEMA Kanda ya Serengeri mkoa wa Simiyu Mara na Shinyanga, Emmanuel Ntobi ametangaza nia ya kugombea ubunge katika Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Ntobi ametangaza leo Jumamosi Juni 27,2020 kuanza mbio za kuusaka ubunge kupitia CHADEMA akieleza kuwa atashukuru endapo Chama chake kitampa ridhaa ya kuwa mgombea Ubunge katika uchaguzi  Mkuu wa Tanzania mwaka 2020.

"Naamini katika nguvu na mamlaka ya umma 'The People's Power' katika kumiliki, kuendesha,kubuni na kuendeleza maamuzi,mawazo,rasilimali,uchumi na siasa yetu. Shinyanga Deserves Better",amesema Ntobi.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger