Tuesday, 23 June 2020

RC Kagera Aagiza Watumishi Wanne Kusimamishwa Kazi, Na Watendaji 30 Kukamatwa Wilayani Biharamulo Kwa Ubadhilifu Wa Milio 307.

...
Na Allawi kaboyo.
Mkuu wa Mkoa Kagera Brig.Jen. Marco Gaguti amemwagiza kamanda wa polisi mkoani humo pamoja na Kamanda wa TAKUKURU kuwakamata watumishi 34 katika halmashauri ya wilaya Biharamulo wakiwemo watendaji wa vijiji na kata kwa kushindwa kurejesha fedha shiligi milioni 307 zilizokusanywa kutoka vyanzo vya mapato ya ndani bila kupelekwa Benki.

Agizo hilo amelitoa juni 23 mwaka huu alipofanya ziara ya kikazi wilayani humo kilicholenga kutoa maelekezo ya kiutendeji kutokana na halmashauri hiyo kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato na kuoneka kunaubadhilifu wa fedha za serikali.

Mku huyo pia licha ya kuagiza kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi watumishi hao, ameziagiza mamlaka kuwasimamisha kazi kaimu mwekahazina Sospiter Makene, Jastine Banula afisa Tehama, Rogers Semukoko afisa tehama na Beatrice Gurusya afisa biashara wote wakiwa ni watumishi wa halmashauri hiyo.

Gaguti amechukua uamuzi huo baada ya kutoa siku saba kwa watumishi hao kurejesha fedha hizo kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika juni 05 mwaka huu kilichokuwa kina lengo la kujibu hoja za mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali.

“Nilikuja hapa nikatoa maelekezo kwa wale wote waliokuwa wanakusanya fedha kwa kutumia mashine za Poss bila kuzipeleka benki kuwa warejeshe fedha na nikawapa siku 7 lakini fedha iliyorejeshwa ni asilimia 2%, kwa mwendo huu hatuwezi kwenda lazima tuweke misingi imara ya kuboresha utumishi na uadilifu, hapa nina orodha ya watendaji 30 ambayo nampati kamanda wa polisi kuhakikisha watu hao wanakamatwa popote walipo na wengine wane hawa naagiza wasimamishwe kazi lakini wawe chini ya uangalizi wa kamati ya ulizi na usalama ili kutoa ushirikiano.” Amefafanua Mkuu wa mkoa Gaguti.

Ameongeza kuwa watumishi wa umma wanatakiwa kuwa waadilifu na kuiogopa fedha ya serikali na kuahidi kuwachukulia hatua wote watakao bainika wakifanya vitendo vya ubadhilifu na kutoa onyo kali kwa watendaji wa vijiji na kata mkoani humo kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato ya serikali bila kuleta ujanjajanja.

“Fedha ya serikali ni ya moto hivyo haipaswi kulala niwasihi tu ndugu zangu tusijaribiane, hatutasita kumchukulia hatua yeyote atakayehusika na upotevu wa pesa, tambueni watendaji ndiyo mnadhamana ya kukusanya mapato ya ndani kutoka katika vyanzo vya mapato katika maeneo yenu.” Ameeleza Gaguti.

Aidha Gaguti amesema kuwa kuna baadhi ya watumishi walikataa kusajili vyanzo vya mato kwa makusudi na baadae kuwarudi wafanyabiashara na kuchukua fedha kinyemela na kusababisha serikali kukosa mapato yake.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger