Tuesday 2 June 2020

MWIZI ARUKA GETI NA KUIBA NYUMBANI KWA MWANDISHI WA ITV,...ASINZIA PAPO HAPO

...

Mwizi aliyekutwa ndani ya gari la Mwandishi wa Habari wa ITV Zanzibar, Farouk Karim.

Mwandishi wa Habari wa ITV Zanzibar, Farouk Karim, amesema kuwa siri kubwa ambayo mtu yeyote anaweza kuifanya ili wezi watakapofika nyumbani kwake waibe lakini wapitiwe na usingizi hapo hapo ni kumuamini na kumuomba Mungu ili awalinde wote ndani ya familia.

Farouk ameyabainisha hayo leo Juni 2, 2020, wakati wa mazungumzo mubashara kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio, na ndipo aliposimulia mkasa wake baada ya mwizi kuruka geti la nyumba yake huko Fuoni visiwani Zanzibar na kuiba nguo na viatu lakini baadaye aliingia ndani ya gari na kupitiwa usingizi. 

"Huyu mwizi kaingia usiku wa manane karuka geti, na hatuna mlinzi pale nyumbani, kakusanya zile nguo zilizokuwa zimeanikwa kaziwekwa kwenye mfuko, katika magari yaliyokuwepo pale gari moja lilikuwa wazi akaingia, akapitia mlango wa abiria akachukua power window, akaenda upande wa dereva kuchukua power window ikamshinda ndiyo akalala hapo hapo" amesema Farouk Karim.

Akielezea siri ya mwizi kumuibia na kisha kupitiwa na usingizi Farouk amesema,"Tumempeleka Polisi kama ambavyo huwa tuna msindikiza Bi harusi, na ile kulala huenda kaiba sana hivyo karidhika, na dawa kubwa ya kumfanya mwizi alale ni moja tu kumuomba Mungu akulinde wewe na nyumba yako, na watu kama sisi ambao hatuna madhambi, Dua zinakubalika, kama unataka hiyo Dua nitafute inbox".
Chanzo - EATV
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger