Wazazi na Walezi Mkoani Shinyanga wametakiwa kuchukua tahadhari kwa watoto wao dhidi ya wanyama aina ya Fisi ambao wamekuwa wakionekana katika maeneo mbalimbali na kusababisha madhara kwao ikiwemo ya vifo.
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba June 2 wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na tukio la kushambuliwa hadi kufariki dunia kwa mtoto wa miaka miwili na nusu aliyehamika kwa jina la Charles Christian katika kitongoji cha Mwagala kata ya Ibadakuli.
Amesema tukio hilo limetokea June Mosi mwaka huu majira ya saa moja usiku akiwa anacheza na watoto wenzake nje ya nyumba yao alijeruhiwa kwa kung'atwa na fisi sehemu za usoni na kisha kuburuzwa umbali wa mita 50 ndipo wananchi walipoamua kumfukuza akamuachia na kukimbia baada ya kuzidi kwa kelele za wananchi hao.
“Wanyama hawa wamekuwa wakizurura ovyo hivyo ni Budi kila mzazi /Mlezi kuhakikisha watoto wao wanakuwa salama na kwani matukio ya watu kushambuliwa na fisi ama mifugo yamekuwa ni mengi hivyo chukueni Tahadhari,”alisema Magiligimba.
Amefafanua kuwa Charles alifariki dunia akiwa njiani akisafirishwa kwenda katika hospitali ya rufaa ya kanda ya Bugando jijini Mwanza kwa matibabu na mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga kwaajili ya kukabidhiwa ndugu zake kwaajili ya Matibabu.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment