Thursday 4 June 2020

JNHPP MW 2115, uchimbaji kina cha lango la kuingilia maji kwenye mitambo wakamilika.

...
Ujenzi wa eneo la lango (Water Intake) la kuingilia maji kwenda kwenye mitambo ya kufua umeme katika Mradi wa Julius Nyerere (Mw 2115) unatarajiwa kukamilika Februari 2022.

Mhandisi Dismas Mbote, Mhandisi wa ujenzi njia za maji pamoja na Bwawa kwenye Mradi wa Julius Nyerere amesema utekelezaji wa njia hiyo ulianza Mwezi Oktoba 2019.

Aliongeza kuwa kazi ya uchimbaji wa lango imekamilika kwa kuchimbwa kina cha mita 53 ambapo hivi sasa kazi inayoendelea ni uondoaji wa kifusi na uchimbaji wa mahandaki matatu yatakayotumika kupitisha maji.

“Vifusi ambavyo vinachimbwa katika mradi huu wa Julius Nyerere havitupwi, mawe yanasagwa na kuwa mchanga, kokoto na mawe mbalimbali ambayo hutumika kwenye ujenzi”, alisema Mhandisi Mbote.

Aidha, zitafanyika kazi za kuchoronga miamba pamoja na kuimarisha kuta kwa zege.

Maji yatakayo fua umeme kabla ya kwenda kwenye mitambo ya kufua umeme yataingia kwanza kwenye lango.

Pia kwa hivi sasa imeletwa mashine ya kuchoronga miamba ambayo ni ya kwanza kwa Tanzania na inayotarajiwa kuongeza kasi katika uchimbaji wa mahandaki ya kupeleka maji kwenye mitambo.

Handaki la kwanza litakuwa na urefu wa mita 350, la pili mita 410 na la tano mita 570 hadi kwenye mitambo ya kufua umeme.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger