Saturday, 16 May 2020

Vifo Vya Corona Marekani Vyafika 88,507.....Trump Anadai Anamatumaini Chanjo Itapatikana Mwishoni Mwa Mwaka Huu

...
Rais Donald Trump wa Marekani amesema serikali yake itawekeza kwa makampuni yote makubwa yanayofanya jitihada za kutafuta chanjo ya virusi vya corona na kwamba imepunguza idadi ya makampuni hayo hadi kufikia 14, huku akitoa ahadi ya kuyapunguza zaidi.

Katika mkutano wake uliofanyikia Ikulu ya Marekani, ambapo ulihudhuriwa na maafisa wengi wa Ikulu hiyo wakiwa wamevaa barakoa, lakini yeye akiwa hajavaa, Trump alionesha matumaini kwamba kinga ya maradhi ya COVID-19  itapatikana kabla ya kumalizika mwaka huu.

Na kuongeza kusema serikali yake itashiriki vyema katika usambazaji wa chanjo hiyo pale tu, itakapopatikana. 

Hayo yanajiri wakati takwimu mpya zilizotolewa na chuo kikuu cha John Hopkins zinaonesha vifo vipya 1,680 ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliopita na kufanya idadi ya vifo kufika 88,507.

Maambukizi nchini Marekani yamefika  1,484,287  na waliopona ni 327,751


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger