Thursday, 21 May 2020

Mume Mbaroni Kwa Kumuwekea Mkewe Pilipili Sehemu za Siri

...
Polisi  katika Kaunti ya Taraka Nithi nchini kenya, wanamshikilia mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la James Muriuki, kwa tuhuma za kumwekea mke wake pilipili kwenye sehemu zake za siri na kisha kumziba na gundi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mei 21, 2020, na Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini humo, imeeleza kuwa mtuhumiwa alikamatwa akiwa mafichoni katika Kaunti ya Kitui, alipotorokea baada ya kutekeleza uhayawani huo.

Imeelezwa kuwa tukio hilo alilitekeleza Mei 16 mwaka huu, ambapo mke wake huyo aliokolewa na majirani waliompeleka hospitalini akiwa na hali mbaya.

Ofisi ya DCI imesema kuwa James Muriuki aliweka pilipili na chumvi, katika nyeti za mke wake huyo kwa kutumia kisu, kabla ya kumziba na gundi, ambapo mara baada ya uchunguzi kukamilika hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger